9/05/2017

Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, maombi

 Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa nini unamwamini Mungu? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa mbinguni, jambo linaloonyesha kwamba wanamwamini Mungu sio ili wamtii, bali kupata manufaa fulani, au kuepuka mateso ya janga. Wakati huo tu ndipo wanakuwa watii kwa kiasi fulani, lakini utii wao ni wa masharti, ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe, na kushinikiziwa. Hivyo: kwa nini unamwamini Mungu? Ikiwa ni kwa ajili ya matarajio yako tu, na majaliwa yako, basi ni bora zaidi usingeamini. Imani kama hii ni kujidanganya, kujihakikishia, na kujishukuru. Kama imani yako haijajengwa katika msingi wa utii kwa Mungu, basi hatimaye utaadhibiwa kwa kumpinga Mungu. Wale wote ambao hawatafuti utii kwa Mungu kwa imani yao wanampinga Mungu. Mungu anaomba kwamba watu watafute ukweli, kwamba wawe na kiu ya neno la Mungu, na wanakula na kunywa maneno ya Mungu, na kuyaweka katika matendo, ili waweze kupata utii kwa Mungu. Kama motisha zako ni hizo kweli, basi Mungu atakuinua juu hakika, na hakika Atakuwa mwenye neema kwako. Hakuna anayeweza kutilia shaka hili, na hakuna anayeweza kulibadilisha. Ikiwa motisha zako sio kwa ajili ya utii kwa Mungu, na una malengo mengine, basi yote ambayo unasema na kufanya—maombi yako mbele ya Mungu, na hata kila tendo lako—litakuwa linampinga Mungu. Unaweza kuwa unaongea kwa upole na mwenye tabia ya upole, kila tendo lako na yale unayoyaonyesha yanaweza kuonekana ni sahihi, unaweza kuonekana kuwa mtu anayetii, lakini linapofikia suala la motisha zako na mitazamo yako juu ya imani kwa Mungu, kila kitu unachofanya kipo kinyume cha Mungu, na ni uovu. Watu wanaoonekana watii kama kondoo, lakini mioyo yao inahifadhi nia mbovu, ni mbwa mwitu katika ngozi ya kondoo, wanamkosea Mungu moja kwa moja, na Mungu hatamwacha hata mmoja. Roho Mtakatifu atamfichua kila mmoja wao, ili wote waweze kuona kwamba kila mmoja wa hao ambao ni wanafiki hakika watachukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu. Usiwe na shaka: Mungu atashughulika na kumkomesha kila mmoja.
Kama huwezi kukubali nuru mpya ya Mungu, na huwezi kuelewa yote ambayo Mungu anayafanya leo, na huyafuati, au unayatilia shaka, unayahukumu, au unayachunguza na kuyachambua, basi huna akili ya kuweza kutii. Kama, nuru ya hapa na sasa inatokea, na bado unathamini nuru ya jana na kuipinga kazi mpya ya Mungu, basi wewe si chochote zaidi ya utani, ni mmoja wa wale wanaompinga Mungu kwa makusudi. Jambo muhimu katika kumtii Mungu ni kuitambua nuru mpya, na kuweza kuikubali na kuiweka katika vitendo. Huu pekee ndio utii wa kweli. Wale ambao hawana hiari ya kuwa na kiu ya Mungu hawana uwezo wa kuwa na akili ya kumtii Mungu, na wanaweza tu kumpinga Mungu kama matokeo ya kuridhika kwao na jinsi hali ilivyo. Kwamba mtu hawezi kumtii Mungu ni kwa sababu amefungwa na kitu kilichotangulia kabla. Mambo ambayo yalikuja kabla yamewapatia watu kila namna ya dhana na njozi za uongo kuhusu Mungu ambazo zimekuwa ndiyo taswira ya Mungu akilini mwao. Hivyo, kile wanachoamini ni dhana zao wenyewe, na viwango vya mawazo yao wenyewe. Ikiwa utampima Mungu ambaye anafanya kazi halisi leo dhidi ya Mungu wa mawazo yako mwenyewe basi imani yako inatoka kwa Shetani, na ni kulingana na mapendeleo yako mwenyewe—na Mungu hataki imani kama hii. Bila kujali sifa zao ni za juu sana kiasi gani, na bila kujali kujitoa kwao—hata kama wamejitoa jitihada za maisha yao yote katika kazi Yake, na wamejitoa mhanga—Mungu hakubali imani yoyote kama hii. Anawaonyesha tu neema kidogo, na kuwaacha waifurahie kwa muda. Watu kama hawa hawawezi kuuweka ukweli katika vitendo, Roho Mtakatifu hafanyi kazi ndani yao, na badala yake Mungu atamwondoa kila mmoja wao. Bila kujali ama ni wazee au vijana, wale ambao hawamtii Mungu katika imani yao na wana motisha mbaya, ni wale ambao wanapinga na kuingilia, na watu kama hao bila kuhoji wataondolewa na Mungu. Wale ambao hawana utii kwa Mungu hata kidogo, ambao wanalitambua tu jina la Mungu, na wana ufahamu kiasi juu ya mapenzi na wema wa Mungu lakini hawaenendi sawa na hatua za Roho Mtakatifu na hawatii kazi na maneno ya sasa ya Roho Mtakatifu—watu kama hao wanaishi katikati ya neema ya Mungu, na hawatachukuliwa na kukamilishwa na Mungu. Mungu huwakamilisha watu kupitia utii wao, kupitia kula kwao, kunywa na kufurahia maneno ya Mungu, na kupitia mateso na usafishaji maishani mwao. Ni kupitia tu imani kama hii ndipo tabia za watu zinaweza kubadilika, baada ya hapo tu ndipo wanaweza kuwa na maarifa ya kweli kuhusu Mungu. Kutoridhika na kuishi katikati ya neema za Mungu, kuwa na kiu ya ukweli, na kutafuta ukweli, na kunuia kuchumwa na Mungu—hii ndio maana ya kumtii Mungu katika hali ya utambuzi; hii ndiyo aina ya imani ambayo Mungu anataka. Watu ambao hawafanyi kitu zaidi ya kufurahia neema za Mungu hawawezi kukamilishwa, au kubadilishwa, na utii wao, uchaji Mungu, na upendo na ustahimilivu vyote hivyo ni vya juujuu tu. Wale ambao wanafurahia tu neema za Mungu hawawezi kumfahamu Mungu kweli, na hata pale wanapomjua Mungu, maarifa yao ni ya juujuu, na wanasema mambo kama vile Mungu anampenda mwanadamu, au Mungu ni mwenye huruma kwa mwanadamu. Hii haiwakilishi maisha ya mwanadamu, na haionyeshi kwamba kweli watu wanamjua Mungu. Ikiwa, maneno ya Mungu yatakapowasafisha, au majaribu yake yatakapowajia, watu hawataweza kumtii Mungu—ikiwa, badala yake, watakuwa watu wa mashaka na kuanguka chini—basi hawana utii hata kidogo. Ndani yao, kuna kanuni na masharti mengi kuhusu imani kwa Mungu, uzoefu wa zamani ambao ni matokeo ya miaka mingi ya imani, au mafundisho mbalimbali kutoka kwenye Biblia. Je, watu kama hawa wanaweza kumwamini Mungu? Watu hawa wamejawa na mambo ya wanadamu—wanawezaje kumtii Mungu? Wote wanatii kulingana na mapendeleo yao binafsi—je, Mungu anaweza kutamani utii kama huu? Huku sio kumtii Mungu bali ni kufungamanishwa na mafundisho, ni kujiridhisha na kujifariji mwenyewe. Ikiwa unasema kwamba huu ni utii kwa Mungu, je, hivi hutakuwa unamkufuru Yeye? Wewe ni Farao wa Misri, unafanya uovu, unajishughulisha katika kazi ya kumpinga Mungu—je, Mungu anaweza kutaka kazi kama hii? Ni bora ungefanya haraka ukatubu na kuweza kujitambua kiasi fulani. Ikiwa sivyo, ni bora uende nyumbani: hivyo itakuwa imekusaidia sana kuliko huduma yako kwa Mungu, hutaingilia wala kusumbua, utakuwa umeijua sehemu yako, na kuishi vizuri—na hiyo haitakuwa bora zaidi? Kwa namna hiyo utakuwa umeepuka kumpinga Mungu na kuweza kuadhibiwa!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguChanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni