11/01/2019

19. Unafiki ni nini?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,Biblia,

19. Unafiki ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:
Ufafanuzi wa neno “Mfarisayo” ni upi? Ni mtu ambaye ni mnafiki, ambaye ni bandia na anajifanya katika kila kitu anachofanya, akijifanya kuwa mwema, mwenye fadhila, na mzuri. Je, hivyo ndivyo alivyo kwa kweli? Yeye ni mnafiki, na hivyo kila kitu kinachodhihirika na kufichuliwa ndani yake ni cha uongo, yote ni kujifanya—sio hali yake ya kweli.

10/24/2019

15. Kwa nini makanisa yanaweza kupotoka na kuwa dini?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,Kazi ya Mungu,

15. Kwa nini makanisa yanaweza kupotoka na kuwa dini?

Maneno Husika ya Mungu:
Kwa nini inasemekana kwamba vitendo vya walio katika makanisa ya kidini vimepitwa na wakati? Ni kwa kuwa wanayoyaweka katika vitendo ni tofauti na kazi ya leo. Katika Enzi ya Neema, walichotenda kilikuwa sahihi, ila kwa kuwa enzi yenyewe imepita na kazi ya Mungu kubadilika, vitendo vyao hatua kwa hatua vimepitwa na wakati. Vimeachwa nyuma na kazi mpya na mwangaza mpya.

10/22/2019

14. Kujihusisha katika sherehe ya kidini ni nini?

14. Kujihusisha katika sherehe ya kidini ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:
Maisha ya kawaida ya kiroho hayakomi tukwa ombi, wimbo, maisha ya kanisa, kula na kunywa maneno ya Mungu, na matendo mengine kama haya, bali yana maana ya kuishi maisha ya kiroho yaliyo mapya na ya kusisimua. Siyo kuhusu mbinu, lakini matokeo. Watu wengi sana wanafikiri kwamba ili kuwa na maisha ya kawaida ya kiroho lazima mtu asali, aombe, ale na anywe Maneno ya Mungu, au kujaribu kuelewa maneno ya Mungu.

10/20/2019

13. Kuna tofauti ipi kati ya kuuelewa ukweli na kuyaelewa mafundisho?

13. Kuna tofauti ipi kati ya kuuelewa ukweli na kuyaelewa mafundisho?

Maneno Husika ya Mungu:
Kupata ufahamu wa kweli kuhusu maana halisi katika Maneno ya Mungu sio jambo rahisi. Usifikiri tu kwamba ikiwa unaweza kutafsiri maana halisi ya maneno ya Mungu, na kila mtu akisema ni vizuri na kukupa hongera inahesabika kama kuelewa, Neno la Mungu. Hilo si sawa na kuelewa neno la Mungu.

10/18/2019

12. Ni nini maana ya “acha kila kitu nyuma na kumfuata Mungu”?

12. Ni nini maana ya “acha kila kitu nyuma na kumfuata Mungu”?

Maneno Husika ya Mungu:
Unaweza kuutoa moyo wako na mwili na upendo wako wote wa kweli kwa Mungu, uyaweke mbele Zake, kuwa mtiifu kabisa Kwake, na kufikiria kabisa mapenzi Yake. Si kwa ajili ya mwili, si kwa ajili ya familia, wala si kwa ajili ya matamanio yako mwenyewe, bali ni kwa ajili ya maslahi ya nyumba ya Mungu. Katika kila kitu unaweza kuchukua Neno la Mungu kama kanuni, kama msingi.

10/16/2019

11. Kuna tofauti ipi kati ya mtu kutekeleza wajibu wake na kutoa huduma?

11. Kuna tofauti ipi kati ya mtu kutekeleza wajibu wake na kutoa huduma?

Maneno Husika ya Mungu:
Hakuna uhusiano kati ya wajibu wa mwanadamu na endapo amebarikiwa au amelaaniwa. Wajibu ni kile ambacho mwanadamu anapaswa kutimiza; ni wajibu wake na hautegemei fidia, masharti, au sababu. Hapo tu ndipo huko kutakuwa kufanya wajibu wake. Mwanadamu aliyebarikiwa hufurahia wema baada ya kufanywa mkamilifu baada ya hukumu.

10/14/2019

10. Mtu kutekeleza wajibu wake ni nini?

10. Mtu kutekeleza wajibu wake ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:
Kutimiza wajibu wako ni ukweli. Kutimiza wajibu wako katika nyumba ya Mungu sio tu kutimiza masharti fulani au kufanya kitu unachopaswa kufanya. Ni kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa anayeishi kati ya mbingu na dunia! Ni kutimiza majukumu na wajibu wako mbele ya Bwana wa uumbaji. Majukumu haya ni majukumu yako ya kweli.