7/21/2019

1. Kuokolewa ni nini? Wokovu ni nini?

VI. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kuokolewa Katika Enzi ya Neema na Wokovu katika Enzi ya Ufalme

1. Kuokolewa ni nini? Wokovu ni nini?


Aya za Biblia za Kurejelea:

“Yule ambaye anaamini na kubatizwa ataokolewa; lakini yule ambaye haamini atahukumiwa” (Marko 16:16).

“Kwa kuwa hii ni damu yangu ya agano jipya, ambayo inamwagwa kwa ajiki ya msamaha wa dhambi” (Mathayo 26:28).

“Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni” (Mathayo 7:21).

Maneno Husika ya Mungu:

Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote. Dhambi za wote ambao walimwamini zilisamehewa; ilimradi wewe ulimwamini, Angeweza kukukomboa wewe; kama wewe ulimwamini Yeye, wewe hukuwa tena mwenye dhambi, wewe ulikuwa umeondolewa dhambi zako. Hii ndiyo ilikuwa maana ya kuokolewa, na kuhesabiwa haki kwa imani. Hata hivyo, kati ya wale walioamini, kulibaki na kitu ambacho kilikuwa na uasi na pingamizi kwa Mungu, na ambacho kilibidi kiondolewe polepole. Wokovu haukuwa na maana kuwa mwanadamu alikuwa amepatwa na Yesu kabisa, lakini ni kuwa mwanadamu hakuwa tena mwenye dhambi, na kuwa alikuwa amesamehewa dhambi zake; mradi tu uliamini, wewe kamwe hungekuwa mwenye dhambi.

kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Wanadamu walipaswa tu kumpokea Yesu Kristo kama Mwokozi ili dhambi zao ziweze kusamehewa. Yaani, dhambi za wanadamu hazikuwa tena kizuizi cha kuufikia wokovu wake na kuja mbele za Mungu na hazikuwa tena nguvu za kushawishi ambazo Shetani alitumia kumlaumu mwanadamu. Hii ni kwa sababu Mungu Mwenyewe Alikuwa Amefanya kazi halisi, na kuwa katika mfano na limbuko la mwili wenye dhambi, na Mungu mwenyewe Alikuwa sadaka ya dhambi. Kwa njia hii, mwanadamu alishuka kutoka msalabani, akiwa amekombolewa na mwili wa Mungu, mfano wa huu mwili wa dhambi.

kutoka katika “Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee” katika Neno Laonekana katika Mwili

Hatua ya siku za mwisho, ambapo mwanadamu atashindwa, ni hatua ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na pia kazi ya wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Maana ya ndani ya ushindi wa mwanadamu ni kurudi kwa mfano halisi wa Shetani, mtu ambaye amepotoshwa na Shetani, kwa Muumba baada ya ushindi wake, kwa njia ambayo atamwacha Shetani na kurejea kabisa kwa Mungu. Kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa.

kutoka katika “Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mwili wa mwanadamu ni wa Shetani, umejaa tabia za kutotii, ni mchafu ya kusikitisha, ni kitu kichafu. Watu hutamani raha ya mwili kupita kiasi, kuna maonyesho mengi sana ya mwili, na kwa hiyo Mungu hudharau mwili kwa kiwango fulani. Watu wanapoacha uchafu, mambo potovu ya Shetani, wao hupata wokovu wa Mungu. Lakini wakibaki bila kuweza kuachana na uchafu na upotovu, basi bado watamilikiwa na Shetani. Kula njama, udanganyifu, na uhalifu wa watu ni mambo ya Shetani; kwa kukuokoa wewe, Mungu hukutenganisha na mambo haya na kazi ya Mungu haiwezi kuwa na kosa, na yote ni kwa sababu ya kuwaokoa watu kutoka gizani. Wakati ambapo umeamini kwa kiwango fulani na unaweza kuachana na upotovu wa mwili, na hufungwi tena na upotovu huu, je, hutakuwa umeokolewa? Wakati ambapo unaishi ukimilikiwa na Shetani huwezi kumdhihirisha Mungu, wewe ni kitu kichafu, na hutapokea urithi wa Mungu. Mara tu umetakaswa na kufanywa kamili, utakuwa mtakatifu, na utakuwa wa kawaida, na utabarikiwa na Mungu na wa kufurahisha kwa Mungu.

kutoka katika “Utendaji (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Wale ambao, katika kazi ya Mungu, wanaweza kukubali jaribio Lake, kukubali ukuu Wake, kujinyenyekeza katika mamlaka Yake, na kufaidi kwa utaratibu hali halisi waliyopitia na matamshi Yake, watakuwa wametimiza maarifa halisi ya mamlaka ya Mungu, ufahamu halisi wa ukuu Wake, na watakuwa kwa kweli watakuwa wanatii Muumba. Watu kama hao tu ndio watakaokuwa wameokolewa kwa kweli.

kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ikiwa mtu anaweza kweli kuingia katika ukweli wa maneno ya Mungu kutokana na mambo na maneno yanayohitajika na Yeye, basi atakuwa mtu aliyekamilishwa na Mungu. Inaweza kusemekana kuwa kazi na maneno ya Mungu yanafaa kabisa kwa mtu huyu, kwamba maneno ya Mungu yanakuwa maisha yake, anapata ukweli, na anaweza kuishi kulingana na maneno ya Mungu. Baada ya hili asili ya mwili wake, yaani, msingi wa kuwepo kwake kwa asili, utatikisika na kuanguka. Baada ya mtu kuwa na maneno ya Mungu kama maisha yake anakuwa mtu mpya. Maneno ya Mungu yanakuwa maisha yake; maono ya kazi ya Mungu, matakwa yake kwa mwanadamu, ufunuo wake kwa mwanadamu, na viwango vya maisha ya kweli ambayo Mungu anahitaji mwanadamu kutimiza vinakuwa maisha yake—anaishi kulingana na maneno haya na ukweli huu, na mtu huyu anageuka kukamilishwa na maneno ya Mungu. Anapitia kuzaliwa upya na anakuwa mtu mpya kupitia maneno Yake.

kutoka katika “Jinsi ya Kuishika Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Ukweli wa leo unatolewa kwa wale ambao wanautamani na kuutafuta. Wokovu huu unapewa wale ambao wanatamani kuokolewa na Mungu, na haujakusudiwa kuwafaidi tu, lakini ili pia ili mpatwe na Mungu. Mnampata Mungu ili Mungu pia awapate. Leo nimenena hayo maneno kwenu, na mmeyasikia, na mnafaa kutenda kulingana na maneno haya. Mwishowe, mkiweka maneno haya katika matendo ndipo nitakapowapata nyinyi kupitia katika maneno haya; na pia, mtakuwa mmepata maneno haya, kumaanisha, mtakuwa mmepata wokovu mkuu. Punde mtakapofanywa wasafi, mtakuwa mmekuwa wanadamu halisi.

kutoka katika “Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Watu wakipitia hadi siku ifike ambapo mtazamo wao wa maisha, na umuhimu na msingi wa kuwepo kwao yamebadilika kabisa, wakati wamebadilishwa kabisa, na wamekuwa mtu mwingine, je, jambo hili halitakuwa la kushangaza? Haya ni mabadiliko makubwa, mabadiliko ya kushangaza sana. Ni wakati tu ambapo hujali umaarufu na utajiri, hadhi, pesa, starehe, na anasa za dunia, na unaweza kuziacha kwa urahisi, ndipo utakuwa na mfanano wa binadamu. Wale ambao watafanywa kamili hatimaye ni kundi kama hili; wataishi kwa ajili ya ukweli, kuishi kwa ajili ya Mungu, na kuishi kwa ajili ya kile ambacho ni cha haki. Buu ndio mfanano wa binadamu wa kweli.

kutoka katika Ushirika wa Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni