1/24/2019

Nyimbo za Dini | 230. Dunia Yote Itashangalia na Kumsifu Mungu

I
Ho~ ho~ ho~ ho~
Yule Mungu mmoja wa kweli ambaye huvitawala vitu vyote katika ulimwengu
—Kristo mwenye uweza!
Huyu ni shahidi wa Roho Mtakatifu.
Anafanya kazi ili kushuhudia kila mahali.
Hivyo hakuna atakayekuwa na shaka yoyote. Mfalme mshindi,
Mwenyezi Mungu, ameushinda ulimwengu.
Ameishinda dhambi na kutimiza ukombozi.
Msifuni Mfalme mshindi wa ulimwengu. 
Dunia nzima itashangalia! Mwenyezi Mungu, wa kustahili sifa!
Utukufu na nguvu ziwe Kwako, Mfalme mkuu wa ulimwengu!

II
Yule Mungu mmoja wa kweli ambaye huvitawala vitu vyote katika ulimwengu
Kristo mwenye uweza!
Huyu ni shahidi wa Roho Mtakatifu.
Anafanya kazi ili kushuhudia kila mahali.
Yeye hutuokoa, ingawa sisi ni wapotovu.
Yeye hutukamilisha kutekeleza mapenzi Yake.
Yeye huitawala dunia na kuirudisha kutoka kwa Shetani
na humfukuza Shetani hadi ndani ya shimo la kuzimu.
Dunia nzima itashangalia! Mwenyezi Mungu, wa kustahili sifa!
Utukufu na nguvu ziwe Kwako, Mfalme mkuu wa ulimwengu!

III

Yeye anauhukumu ulimwengu. Hakuna anayeweza kutoka mikononi Mwake.
Yeye hutawala kama Mfalme milele.
Dunia nzima itashangalia! Mwenyezi Mungu, wa kustahili sifa!
Utukufu na nguvu ziwe Kwako, Mfalme mkuu wa ulimwengu!
Dunia nzima itashangalia! Mwenyezi Mungu, wa kustahili sifa!
Utukufu na nguvu ziwe Kwako, Mfalme mkuu wa ulimwengu!

kutoka kwa "Tamko la Ishirini na Saba" katika Neno Laonekana
katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni