11/07/2018

Kiini cha Kristo Ni Mungu


Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Nyimbo



Kiini cha Kristo Ni Mung

I
Mungu anayekuwa mwili anaitwa Kristo,
na hivyo Kristo anayeweza kuwapa watu ukweli anaitwa Mungu.
Si kupita kiasi kusema hivyo,
kwani Ana kiini cha Mungu.
Ana tabia ya Mungu na hekima katika kazi Yake,
ambayo haifikiwi na mwanadamu.
Wale wanaojiita Kristo wenyewe
ilhali hawawezi kufanya kazi
ya Mungu ni wadanganyifu.
Wanaojifanya kuwa Kristo hatimaye wataanguka,
ingawaje wanadai kuwa Kristo,
hawana kiini chochote cha Kristo.

II
Kristo sio tu udhihirisho wa Mungu duniani,
lakini mwili hasa uliochukuliwa na Mungu.
Anapotekeleza na kutimiza kazi Yake kati ya mwanadamu.
Mwili huu hauwezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote tu.
Ila mwili unaoweza kutosha kubeba kazi ya Mungu duniani.
Na kuonyesha tabia ya Mungu,
na kumwakilisha Mungu vizuri na kumpa mwanadamu uzima.
Hivyo Mungu anasema kuwa uhalali wa Kristo,
hauwezi kufafanuliwa na mwanadamu,
lakini unajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe.
Hivyo kama kwa kweli unataka kutafuta njia ya uzima,
lazima kwanza utambue,
ni katika siku za mwisho ambapo Anakuja duniani,
kumpa mwanadamu njia ya uzima.
Sio zamani, sio zamani; inafanyika leo.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni