11/09/2018

4. Ni jinsi gani hatua tatu za kazi ya Mungu kwa pole pole huongeza uketo ili watu waokolewe na kukamilishwa?

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, kazi ya Mungu

4. Ni jinsi gani hatua tatu za kazi ya Mungu kwa pole pole huongeza uketo ili watu waokolewe na kukamilishwa?

Maneno Husika ya Mungu:
Usimamizi mzima wa Mungu umegawika kwa hatua tatu, na katika kila hatua, mahitaji yanayopatana yanatokana na mwanadamu. Aidha, kadri enzi zinavyopita na kuendelea, mahitaji ya Mungu kwa wanadamu huongezeka hata zaidi. Kwa hiyo, hatua kwa hatua, kazi hii ya usimamizi wa Mungu hufikia kilele chake, hadi mwanadamu aamini ukweli wa “kuonekana kwa Neno katika mwili,” na hivyo mahitaji ya mwanadamu huongezeka hata zaidi, na mahitaji ya mwanadamu kutoa ushuhuda huongezeka hata zaidi. … Wakati wa kale, mwanadamu alihitajika kuzingatia sheria na amri, na alihitajika kuwa mpole na mnyenyekevu. Leo, mwanadamu anahitajika kutii mipango yote ya Mungu na awe na upendo mkuu wa Mungu, na zaidi bado anahitajika kumpenda Mungu katika mateso. Hatua hizi tatu ndizo Mungu anazozitazamia toka kwa mwanadamu, hatua kwa hatua, katika usimamizi Wake wote. Kila hatua ya kazi ya Mungu huzidisha kina kuliko iliyopita, na katika kila hatua, mahitaji ya mwanadamu ni makubwa kuliko yaliyopita, na kwa hali hii, umbo la usimamizi mzima wa Mungu huonekana. Ni hasa kwa sababu mahitaji ya mwanadamu kila mara huwa juu kuliko tabia yake inavyoweza kufikia viwango anavyovihitaji Mungu, na ni hapo ambapo wanadamu wataanza kujiondoa polepole kutoka kwa ushawishi wa Shetani, ndipo kazi ya Mungu itafikia kikomo, wanadamu wote watakuwa wameokolewa kutoka kwa ushawishi wa Shetani.
kutoka kwa “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ya usimamizi wa Mungu ilianza Alipoumba ulimwengu, na mwanadamu ni kiini cha kazi Yake. Uumbaji wa Mungu wa kila kitu, unaweza kusemwa, ni kwa ajili ya mwanadamu. Kwa sababu Kazi ya usimamizi Wake imesambaa katika maelfu ya miaka, na haijatekelezwa katika dakika na sekunde tu, ama kufumba na kufumbua, ama katika mwaka mmoja au miwili, ilimbidi Aumbe vitu vingine zaidi kwa ajili ya maisha ya mwanadamu, kama vile jua, mwezi, na aina zote za viumbe walio hai, na chakula na mazingira kwa ajili ya wanadamu. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa usimamizi wa Mungu.
Baada ya hapo, Mungu Alimkabidhi mwanadamu kwa Shetani, mwanadamu aliishi chini ya miliki ya Shetani, na hili taratibu lilisababisha kazi ya Mungu ya enzi ya kwanza: hadithi ya Enzi ya Sheria.... Kipindi cha miaka elfu kadhaa za Enzi ya Sheria, wanadamu walikuwa wazoefu wa maelekezo ya Enzi ya Sheria, na wakaanza kupuuza, na taratibu wakaacha ulinzi wa Mungu. Na hivyo, pamoja na kushikilia sheria, walimwabudu Mungu na kutenda matendo maovu. Walikuwa bila ulinzi wa Yehova, na waliishi tu mbele ya madhabahu ndani ya hekalu. Kwa kweli, Kazi ya Mungu ilikuwa imejitenga nao kitambo sana, na hata kama Waisraeli walijikita katika sheria, na kulitaja jina la Yehova, na kwa majivuno kuamini kuwa wao pekee ndio walikuwa watu wa Yehova na walikuwa wamechaguliwa na Yehova, utukufu wa Mungu uliwaacha kimyakimya …
…………
Kama ilivyokuwa kawaida, baada ya kazi ya Yehova katika Enzi ya Sheria, Mungu Alianza kazi yake ya hatua ya pili: kwa kuutwaa mwili, kuwa na mwili kama binadamu kwa miaka kumi, ishirini, na kuongea na kufanya kazi Yake Kati ya waumini. Na bado bila mapendeleo, hakuna aliyejua, na ni idadi ndogo tu ya watu walitambua kuwa Alikuwa Mungu Aliyepata mwili baada ya Yesu Kristo kupigiliwa misumari msalabani na kufufuka. … Baada tu ya kazi ya Mungu katika hatua ya pili kukamilika—baada ya kusulubishwa—kazi ya Mungu ya kutoa mwanadamu kwenye dhambi (ambayo ni kusema, kumtoa mwanadamu mikononi mwa Shetani) ilitimilika. Na hivyo, kutoka wakati huo kuendelea mbele, wanadamu walipaswa tu kumpokea Yesu Kristo kama Mwokozi ili dhambi zao ziweze kusamehewa. Yaani, dhambi za wanadamu hazikuwa tena kizuizi cha kuufikia wokovu wake na kuja mbele za Mungu na hazikuwa tena nguvu za kushawishi ambazo Shetani alitumia kumlaumu mwanadamu. Hii ni kwa sababu Mungu Mwenyewe Alikuwa Amefanya kazi halisi, na kuwa katika mfano na limbuko la mwili wenye dhambi, na Mungu mwenyewe Alikuwa sadaka ya dhambi. Kwa njia hii, mwanadamu alishuka kutoka msalabani, akiwa amekombolewa na mwili wa Mungu, mfano wa huu mwili wa dhambi. Na hivyo, baada ya kushikwa mateka na Shetani, mwanadamu alikuja hatua moja mbele karibu na kukubali wokovu mbele za Mungu. Kwa hakika, huu ulingo wa kazi ndio ulikuwa usimamizi wa Mungu ambao ulikuwa hatua moja mbali na Enzi ya sheria, na wa kiwango cha ndani kuliko Enzi ya Sheria.
…………
Baadaye kukaja Enzi ya Ufalme, ambayo ni hatua ya utendaji zaidi na bado ni ngumu zaidi kukubalika na mwanadamu. Hii ni kwa sababu jinsi mwanadamu ajavyo karibu na Mungu, ndivyo afikapo karibu na kiboko cha Mungu, na ndivyo uso wa Mungu unavyokuwa wazi mbele ya mwanadamu. Kwa kufuatia kukombolewa kwa wanadamu, mwanadamu kirasmi anarejelea familia ya Mungu. Mwanadamu alifikiria kuwa huu ndio wakati wa kufurahia, bado ameegemezwa kwa shambulizi la Mungu na mifano ya yale bado hayajaonekana na yeyote. Inavyokuwa, huu ni ubatizo ambao watu wa Mungu wanapaswa “kuufurahia." Katika muktadha huo, watu hawana lingine ila kuacha na kujifikiria wao wenyewe, Mimi ndimi mwanakondoo, aliyepotea kwa miaka mingi, ambaye Mungu Amegharamika kumnunua, sasa kwa nini Mungu Ananitendea hivi? Ama ni njia ya Mungu kunicheka, na kunifichua? … Baada ya miaka mingi kupita, mwanadamu amedhoofika, kwa kuupitia ugumu wa usafishaji na kuadibu. Ijapokuwa mwanadamu amepoteza "utukufu" na "mapenzi" ya wakati uliopita, bila ya kufahamu amekuja kuelewa ukweli wa kuwa mwanadamu, na amekuja kutambua kazi ya Mungu ya kujitolea kuokoa wanadamu. Taratibu mwanadamu anaanza kuchukia ushenzi wake mwenyewe. Anaanza kuchukia jinsi alivyo mkali, na lawama kuelekea kwa Mungu, na mahitaji yote yasiyokuwa na mwelekeo aliyodai kutoka Kwake. Wakati hauwezi ukarudishwa nyuma, matendo ya zamani huwa ya kujuta katika kumbukumbu za mwanadamu, na maneno na upendo wa Mungu vinakuwa ndivyo vinavyomwendesha mwanadamu katika maisha Yake mapya. Majeraha ya mwanadamu hupona siku baada ya siku, nguvu humrudia, na akasimama na kutazamia uso Wake mwenye Uweza … ndipo anagundua kuwa daima Ameishi kando yangu, na kwamba tabasamu Lake na sura Yake ya kupendeza bado zinasisimua. Moyo Wake bado unawajali wanadamu Aliowaumba, na mikono Yake bado ina joto na nguvu kama ilivyokuwa hapo mwanzoni. Ni kama mwanadamu alirudi kwenye bustani ya Edeni, lakini wakati huu mwanadamu hasikizi ushawishi wa nyoka, na hatazami kando na uso wa Yehova. Mwanadamu anapiga magoti mbele ya Mungu, na kutazama uso Wake wenye tabasamu, na kumtolea Mungu kafara yenye thamani—Ee! Bwana wangu, Mungu wangu!
kutoka kwa “Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi iliyofanywa na Yesu ilikuwa tu hatua moja juu zaidi ya Agano la Kale; ilitumiwa kuianza enzi, na kuiongoza enzi hiyo. Kwa nini Alisema, "Sikuja kuharibu sheria, bali kuitimiza"? Lakini katika kazi Yake kulikuwa na mengi ambayo yalitofautiana na sheria zilizotumika na amri zilizofuatwa na Waisraeli wa Agano la Kale, kwani Hakuja kuitii sheria, bali kuitimiza. Mchakato wa kuitimiza ulikuwa pamoja na mambo mengi halisi: Kazi Yake ilikuwa ya vitendo zaidi na halisi, na, zaidi ya hayo, ilikuwa hai, na sio tu kufuata mafundisho ya dini bila ufahamu. Je, Waisraeli hawakuitii Sabato? Yesu alipokuja Hakuitii Sabato, kwani Alisema kwamba Mwana wa Adamu alikuwa Bwana wa Sabato, na wakati ambapo Bwana wa Sabato alikuja, Angefanya Alivyopenda. Alikuwa Amekuja kutimiza sheria za Agano la Kale na kuzibadilisha sheria. Yote ambayo hufanywa leo ni kwa msingi wa siku hizi, lakini bado yako juu ya msingi wa kazi ya Bwana katika Enzi ya Sheria, na hayavuki mipaka ya eneo hili. Kuulinda ndimi zenu, na kutozini, kwa mfano—Je, hizi si sheria za Agano la Kale? Leo, kile kinachotakikana kwenu sio chenye upeo wa amri kumi tu, lakini ni amri ambazo zina ukuu kuliko hizo zilizokuwepo hapo awali, ila hii haina maana kuwa kile kilichokuja hapo awali kimeondolewa, kwa kuwa kila awamu ya kazi ya Mungu hufanywa juu ya msingi wa awamu ambayo ilikuja hapo awali. Kile ambacho Yehova aliwasilisha kwa Israeli, kama vile kutoa sadaka, kumheshimu baba na mama yako, kutoabudu sanamu, kutowadhulumu wengine, kutowalaani wengine, kutozini, kutovuta sigara, kutokunywa pombe, kutokula nyamafu, na kutokunywa damu, huo si msingi wa utendaji wenu hata leo? Kazi iliyotekelezwa hadi leo iko juu ya msingi wa mambo ya zamani. Ingawa sheria za zamani hazitajwi tena, nawe umewekewa masharti mapya, sheria hizi hazijafutwa, na badala yake, zimeinuliwa. Kusema kwamba zimefutwa kuna maana kwamba enzi ya awali imepitwa na wakati, lakini kuna amri zingine ambazo lazima uzitii. Amri za zamani tayari zimetiwa katika vitendo, tayari zimekuwa nafsi ya mwanadamu, na hakuna haja ya kurudia kusema amri za kutovuta sigara, kutokunywa pombe, na kadhalika. Juu ya msingi huu, amri mpya zimeagizwa kufuatana na mahitaji yenu leo, kufuatana na kimo chenu, na kufuatana na kazi ya leo. Kutangaza amri kwa ajili ya enzi mpya hakumaanishi kufuta amri za enzi ya kale, bali kuziinua juu zaidi ya msingi huu, kuyafanya matendo ya mwanadamu kuwa kamili zaidi, na kufuatana na uhalisi zaidi. Kama, leo, mngetakiwa tu kufuata amri na kutii sheria za Agano la Kale, kwa namna sawa na wana wa Israeli, na kama, hata, nyinyi mlitakiwa mkariri sheria ambazo ziliwekwa na Bwana, hakungekuwa na uwezekano kwamba mngeweza kubadilika. Kama mngekuwa tu mnatakiwa kutii zile amri chache zilizo na mipaka ama kukariri sheria zisizohesabika, asili zenu za zamani zingebaki zimekita mizizi, na hakungekuwa na mbinu ya kuzing’oa. Hivyo mngeendelea kuzidi kupotoshwa, na hakuna hata mmoja wenu angeweza kuwa mtiifu. Ambayo ni kusema kwamba amri chache rahisi au sheria zisizohesabika hazina uwezo wa kuwasaidia kujua matendo ya Yehova. Nyinyi si sawa na wana wa Israeli: kwa kufuata sheria na kukariri amri waliweza kushuhudia matendo ya Yehova, na kumpa Yeye pekee ibada yao, lakini hamwezi kufanikisha hili, na amri chache za Agano la Kale haziwezi tu kuwafanya nyinyi kupeana mioyo yenu, au kuwalinda, lakini badala yake itawafanya muwe wazembe, na kuwateremsha mpaka Kuzimu. Kwa sababu kazi Yangu ni kazi ya ushindi, na inalenga uasi wenu na asili yenu ya zamani. Maneno yenye huruma ya Yehova na Yesu yanapungukiwa mno na maneno makali ya hukumu leo. Bila maneno makali kama haya, ingekuwa vigumu kuwashinda ninyi “wataalam,” ambao mmekua wasiotii kwa miaka elfu nyingi. Sheria za Agano la Kale zilipoteza nguvu zake kwenu kwa muda mrefu uliopita, na hukumu ya leo ni ya kuogofya mno kuliko sheria za zamani. Ya kuwafaa nyinyi zaidi ni hukumu, na wala si vikwazo duni vya sheria, kwa kuwa ninyi si wanadamu wa mwanzo kabisa, lakini wanadamu ambao wamekuwa fisadi kwa miaka elfu nyingi. Kile ambacho mwanadamu lazima atimize sasa ni kulingana na hali halisi ya mwanadamu leo, kulingana na tabia bora na kimo halisi cha mwanadamu wa siku hizi, na hakihitaji kwamba wewe ufuate mafundisho ya dini. Hii ni kwa minajili ya mabadiliko yaweze kupatikana katika asili zako za zamani, na ili uweze kutupa kando dhana zako.
kutoka kwa “Maono ya Kazi ya Mungu (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ingawa njia ambayo mwanadamu hutembea leo pia ni njia ya msalaba na ya kuteseka, kile ambacho mwanadamu wa leo hutenda, hula, hunywa na hufurahia ni tofauti zaidi na yale ya mwanadamu aliyekuwa chini ya sheria na katika Enzi ya Neema. Kinachohitajika kutoka kwa mwanadamu wakati huu sio kama ilivyokuwa kitambo na zaidi sio kama kilichohitajika kutoka kwake katika Enzi ya Sheria. Na ni kipi kilichoulizwa kwa mwanadamu chini ya Sheria kazi ilipofanya Israeli? Hawakuulizwa cochote zaidi ya kuiheshimu Sabato na Sheria za Yehova. Lakini si hivyo katika wakati huu. Siku ya Sabato, mwanadamu anafanya kazi, hukusanyika na kuomba kama kawaida, na hakuna vizuizi vinavyowekwa. Wale katika Enzi ya Neema ilibidi wabatizwe; sio hilo tu, pia walitarajiwa kufunga, kuvunja mkate, kunywa divai, kufunika vichwa vyao na kuosha miguu yao. Sasa, sheria hizi zimefutwa na mahitaji makuu yanaulizwa kutoka kwa mwanadamu, kwani kazi ya Mungu inaendelea kuimarika na kuingia kwa mwanadamu kunafika kiwango cha juu. Zamani, Yesu Aliweka mikono Yake juu ya mwanadamu na kuomba, lakini sasa kwamba kila kitu kimesemwa, kuwekelea mikono kuna maana gani? Maneno pekee yanaweza kupata matokeo. Alipowekelea mikono Yake juu ya mwanadamu hapo awali, ilikuwa ni kwa ajili ya kumbariki na kumponya mwanadamu. Hivyo ndivyo Roho Mtakatifu Alivyofanya kazi wakati huo, lakini sio hivyo wakati huu. Wakati huu, Roho Mtakatifu Anatumia maneno katika kazi Yake ili kupata matokeo. Ameyafanya maneno Yake wazi kwenu, na mnapaswa tu kuyaweka katika matendo. Maneno Yake ni mapenzi Yake na yanaonyesha kazi Atakayofanya. Kupitia kwa maneno Yake, utaweza kuelewa mapenzi Yake na yale ambayo Anauliza upate. Unayaweka tu maneno Yake katika matendo moja kwa moja bila haja ya kuwekelea mikono. Wengine wanaweza kusema, “Wekelea mikono Yako juu yangu! Wekelea mikono yako juu yangu ili niweze kupokea baraka zako na kushiriki kwako.” Haya yote ni mazoezi yaliyopitwa na wakati na na ambayo yanakataliwa katika wakati huu, kwani enzi zimebadilika. Roho Mtakatifu Anafanya kazi kulingana na enzi, sio tu katika mapenzi Yake ama kulingana na masharti. Enzi zimebadilika, na enzi mpya lazima ilete kazi mpya. Huu ni ukweli wa kila hatua ya kazi, na hivyo kazi Yake haiwezi kurudiwa. Katika Enzi ya Neema, Yesu Alifanya nyingi ya kazi hiyo, kama kuponya magonjwa, kukemea mapepo, kuwekelea mikono Yake juu ya wanadamu, na kumbariki mwanadamu. Hata hivyo, kuendelea kufanya hivyo hakutasaidia chochote katika wakati huu. Roho Mtakatifu Alifanya kazi hivyo katika huo wakati, kwani ilikuwa Enzi ya Neema, na mwanadamu alipewa neema ya kutosha ili afurahie. Mwanadamu hakuhitajika kulipa gharama yoyote na angepokea neema mradi tu angekuwa na imani. Kila mtu alitendewa kwa neema kubwa. Sasa, enzi imebadilika, na kazi ya Mungu imeendelea zaidi; kupitia kuadibu na hukumu Yake, uasi wa mwanadamu na vitu vichafu katika mwanadamu vitatupiliwa mbali. Jinsi ilivyokuwa hatua ya wokovu, ilimbidi Mungu kufanya kazi hiyo, Akimwonyesha mwanadamu neema ya kutosha ili mwanadamu afurahie, ili Amkomboe mwanadamu kutoka kwa dhambi, na kwa neema amsamehe mwanadamu dhambi zake. Hatua hii inafanywa ili kubaini kukoseka kwa usawa katika mwanadamu kupitia kuadibu, hukumu, kupigwa na maneno, na vile vile nidhamu na ufunuo wa maneno, ili baadaye waweze kuokolewa. Hii ni kazi ya undani zaidi kuliko ukombozi. Katika Enzi ya Neema, mwanadamu alifurahia neema ya kutosha na amezoea neema hii, kwa hivyo sio ya kufurahiwa na mwanadamu tena. Kazi kama hii imepitwa na wakati sasa na haitafanyika tena. Sasa, mwanadamu anaokolewa kupitia hukumu ya neno. Baada ya mwanadamu kuhukumiwa, kuadibiwa na kusafishwa, tabia yake basi inabadilika. Je sio kwa sababu ya maneno ambayo Nimenena? Kila hatua ya kazi inafanywa kulingana na maendeleo ya binadamu wote na kwa enzi. Kazi yote ina umuhimu wake; inafanywa kwa ajili ya wokovu wa mwisho, ili binadamu awe na hatima nzuri baadaye, na kwa mwanadamu kugawanywa kulingana na aina Yake mwishowe.
kutoka kwa “Fumbo la Kupata Mwili (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati wa Enzi ya Sheria, Yehova Alimwongoza Musa kutoka Misri kwa maneno Yake, na Akazungumza maneno fulani kwa Wanaisraeli; wakati huo, sehemu ya matendo ya Mungu yaliwekwa wazi, lakini kwa sababu ubora wa tabia ya mwanadamu ulikuwa finyu na hakuna kitu chochote ambacho kingeweza kufanya maarifa yake kukamilika, Mungu Aliendelea kuzungumza na kufanya kazi. Wakati wa Enzi ya Neema, mwanadamu aliweza kuona tena sehemu ya matendo ya Mungu. Yesu Aliweza kuonyesha ishara na maajabu, kuponya wagonjwa na kutoa mapepo, na kusulubishwa, siku tatu baadaye. Akafufuka na Akawatokea watu Akiwa katika mwili. Kumhusu Mungu, mwanadamu hakujua chochote zaidi ya hiki. Mwanadamu anajua tu kile ambacho Mungu Amemwonyesha, na kama Mungu Asingeonyesha chochote zaidi kwa mwanadamu, basi hicho kingekuwa kiwango cha mwanadamu kumwekea mipaka Mungu. Hivyo, Mungu Anaendelea kufanya kazi, ili maarifa ya mwanadamu juu Yake yaweze kuwa ya kina zaidi, na ili taratibu aweze kuijua hulka ya Mungu. Mungu Anatumia maneno Yake kumkamilisha mwanadamu. Tabia yako iliyoharibika imewekwa wazi kwa maneno ya Mungu, na dhana zako za kidini zinaondolewa na uhalisia wa Mungu. Mungu katika mwili wa siku za mwisho Amekuja hasa kwa ajili ya kutimiza maneno haya kwamba "Neno Lafanyika kuwa mwili, Neno Lakuwa mwili, na Neno Lanaonekana katika mwili," na kama huna maarifa ya kina kuhusu hili, basi hutaweza kusimama imara; wakati wa siku za mwisho, kimsingi Mungu Anakusudia kukamilisha hatua ya kazi ambayo kwayo Neno Anaonekana katika mwili, na hii ni sehemu moja ya mpango wa Mungu wa usimamizi. Hivyo, maarifa yako yanapaswa kuwa wazi; bila kujali namna ambavyo Mungu Anafanya kazi, Mungu Hamruhusu mwanadamu kumwekea mipaka. Ikiwa Mungu Asingefanya kazi hii wakati wa siku za mwisho, basi maarifa ya mwanadamu juu Yake yasingeweza kwenda popote. Ungeweza kujua tu kwamba Mungu Anaweza kusulubiwa na Anaweza kuiangamiza Sodoma, na kwamba Yesu Anaweza kufufuliwa kutoka katika wafu na kumtokea Petro.... Lakini usingeweza kusema kwamba maneno ya Mungu yanaweza kutimiza yote, na yanaweza kumshinda mwanadamu. Ni kwa njia tu ya kupitia uzoefu wa maneno ya Mungu ndipo unaweza kuzungumza juu ya maarifa hayo, na kadri unapopitia uzoefu wa kazi ya Mungu zaidi, ndivyo maarifa yako yanavyokuwa ya kina zaidi kumhusu Yeye. Ni baada ya hapo tu ndipo utaacha kumwekea Mungu mipaka ndani ya dhana zako binafsi.
kutoka kwa “Kuijua Kazi ya Mungu Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika kazi ya siku za mwisho, neno ni kubwa zaidi ya udhihirisho wa ishara na maajabu, na mamlaka ya neno yanashinda yale ya ishara na maajabu. Neno linaweka wazi tabia zote potovu katika moyo wa mwanadamu. Huwezi kutambua kivyako wewe mwenyewe. Yatakapofunuliwa kwako kupitia kwa neno, utakuja kujua mwenyewe; hutaweza kuyakataa, na na utashawishika kikamilifu. Je haya si mamlaka ya neno? Haya ndiyo matokeo yanayopatikana kwa kazi ya wakati huu ya neno. Kwa hivyo, mwanadamu hawezi kuokolewa kikamilifu kutoka kwa dhambi zake kwa kuponya magonjwa na kukemea mapepo na hawezi kufanywa mkamilifu kabisa kwa udhihirisho wa ishara na maajabu. Mamlaka ya kuponya na kukemea mapepo yanapatia mwanadamu neema tu, lakini mwili wa mwanadamu bado ni wa Shetani na tabia potovu za kishetani zitabaki ndani ya mwanadamu. Kwa maneno mengine, yale ambayo hayajatakaswa bado ni ya dhambi na uchafu. Ni baada tu ya mwanadamu kufanywa safi kupitia kwa maneno ndipo atakapotwaliwa na Mungu na kutakaswa. Lingine lisipofanywa ila kukemea mapepo katika mwanadamu na kumkomboa, huko ni kumshika tu kutoka kwa mikono ya Shetani na kumrudisha kwa Mungu. Hata hivyo, hajafanywa msafi ama kubadilishwa na Mungu, anabaki mpotovu. Ndani ya mwanadamu bado kuna uchafu, pingamizi na uasi; mwanadamu amerudi tu kwa Mungu kupitia kwa ukombozi, lakini mwanadamu hana maarifa kumhusu na bado anamkataa na kumsaliti Mungu. Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuutupa nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso. Kwa kweli hatua hii ni ile ya ushindi na pia hatua ya pili ya wokovu. Mwanadamu anatwaliwa na Mungu kupitia hukumu na kuadibu na neno; kwa kutumia neno kusafisha, hukumu na kufichua, uchafu wote, fikira, nia, na matumaini ya mtu mwenyewe katika moyo wa mwanadamu zinafuliwa. Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivyo, hata kama sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu. Kwa mfano, wakati ambapo watu walijua kwamba walitoka kwa Moabu, walitoa maneno ya malalamiko, hawakutafuta tena uzima, na wakawa baridi kabisa. Je, hili halionyeshi kwamba bado hawawezi kutii kwa ukamilifu kutawaliwa na Mungu? Je, hii siyo tabia ya kishetani ya upotovu kabisa? Ulipokuwa hupitii kuadibu, mikono yako iliinuliwa juu zaidi ya wengine wote, hata ile ya Yesu. Na ulilia kwa sauti kubwa: Kuwa mwana mpendwa wa Mungu! Kuwa mwandani wa Mungu! Ni heri tufe kuliko kumtii Shetani! Muasi Shetani wa zamani! Liasi joka kuu jekundu! Acha joka kuu jekundu lianguke kabisa kutoka mamlakani! Acha Mungu atufanye kamili! Vilio vyako vilikuwa vikubwa zaidi ya wengine. Lakini kisha zikaja nyakati za kuadibu na, mara tena, tabia ya upotovu ya watu ilifichuliwa. Kisha, vilio vyao vikakoma, na hawakuwa tena na azimio. Huu ni upotovu wa mwanadamu; unaingia ndani zaidi kuliko dhambi, ulipandwa na Shetani na umekita mizizi ndani zaidi ya mwanadamu. Sio rahisi kwa mwanadamu kuzifahamu dhambi zake; mwanadamu hawezi kufahamu asili yake iliyokita mizizi. Ni kupitia tu katika hukumu na neno ndipo mabadiliko haya yatatokea. Hapo tu ndipo mwanadamu ataendelea kubadilika kutoka hatua hiyo kuendelea. Mwanadamu alipiga kelele hivyo wakati uliopita kwa sababu mwanadamu hakuwa na ufahamu wa tabia yake potovu ya asili. Huo ndio uchafu ulio ndani ya mwanadamu. Kotekote katika kipindi kirefu hivyo cha hukumu na kuadibu, mwanadamu aliishi katika mazingira ya mvutano. Je, haya yote hayakutimizwa kupitia kwa neno? Wewe pia hukulia kwa sauti ya juu kabla ya majaribio ya watendaji huduma? Ingia katika ufalme! Wale wote ambao wanalikubali jina hili wataingia katika ufalme! Wote watashiriki Mungu! Wakati ambapo majaribio ya watendaji huduma yalikuja, hukulia tena. Mwanzoni, wote walilia, “Mungu! Popote Uniwekapo, nitatii kuongozwa na Wewe.” Baada ya kusoma maneno ya Mungu, “Nani atakuwa Paulo Wangu?” mwanadamu alisema, “Niko radhi!” Kisha akayaona maneno, “Na kuhusu imani ya Ayubu?” Kwa hiyo akasema, “Niko radhi kuichukua imani ya Ayubu. Mungu, tafadhali nijaribu!” Majaribio ya watendaji huduma yalipokuja, alizirai mara moja na nusura angekosa kusimama tena. Baada ya hilo, uchafu ndani ya moyo wa mwanadamu ulipungua polepole. Je, hili halikutimizwa kupitia kwa neno? Kwa hiyo, kile ambacho mmepitia wakati wa sasa ni matokeo ambayo hutimizwa kupitia kwa neno, hata makuu zaidi ya yale ambayo hutimizwa kupitia kwa Yesu kufanya ishara na maajabu. Utukufu wa Mungu na mamlaka ya Mungu Mwenyewe ambayo ninyi huona hayaonekani tu kupitia kwa usulubishaji, uponyaji wa magonjwa na ufukuzaji wa pepo, lakini zaidi kupitia kwa hukumu Yake kwa neno. Hili hukuonyesha wewe kwamba sio tu ufanyaji wa ishara, uponyaji wa magonjwa na ufukuzaji wa pepo ndiyo mamlaka na nguvu za Mungu, bali hukumu kwa neno unaweza kuwakilisha bora mamlaka ya Mungu na kufichua uweza Wake.
kutoka kwa “Fumbo la Kupata Mwili (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika kazi ya wokovu wa mwanadamu, awamu tatu zimefanywa, ambayo ni kusema kuwa vita na Shetani vimegawanyika katika awamu tatu kabla ya kushindwa kabisa kwa Shetani. Na bado ukweli wa ndani wa kazi yote ya vita dhidi ya Shetani ni kwamba matokeo yake yanatimizika kupitia kuzawadia mwanadamu neema, na kuwa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, kuzisamehe dhambi za mwanadamu, kumshinda mwanadamu, na kumfanya mwanadamu awe kamili. Kama jambo la kweli, vita na Shetani sio kuchukua silaha dhidi ya Shetani, bali ni wokovu wa mwanadamu, kuyashughulikia maisha ya mwanadamu, na kubadilishwa kwa tabia ya mwanadamu ili kwamba aweze kuwa na ushahidi wa Mungu. Hivi ndivyo Shetani anashindwa. Shetani anashindwa kwa kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Wakati Shetani ameshindwa, yaani, wakati mwanadamu ameokolewa kabisa, basi Shetani aliyeaibika atafungwa kabisa, na kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kiini cha wokovu wa mwanadamu ni vita dhidi ya Shetani, na vita na Shetani vitajitokeza kimsingi katika wokovu wa mwanadamu. Awamu ya siku za mwisho, ambapo mwanadamu atashindwa, ni awamu ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na pia kazi ya wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa utawala wa Shetani. Maana ya ndani ya ushindi wa mwanadamu ni kurudi kwa mfano halisi wa Shetani, mtu ambaye amepotoshwa na Shetani, kwa Muumba baada ya ushindi wake, kwa njia ambayo atamwacha Shetani na kurejea kabisa kwa Mungu. Kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni kazi ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na awamu ya mwisho ya kazi ya Mungu ya usimamizi kwa ajili ya kushindwa kwa Shetani. Bila kazi hii, wokovu kamili wa mwanadamu hatimaye haungewezekana, kushindwa kikamilifu kwa Shetani kusingewezekana, na mwanadamu kamwe hangekuwa na uwezo wa kuingia kwenye hatima ya ajabu, ama kuwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kwa hivyo, kazi ya wokovu wa mwanadamu haiwezi kukamilika kabla vita dhidi ya Shetani havijahitimishwa, kwa kuwa msingi wa kazi ya Mungu wa usimamizi ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Mwanadamu wa kwanza kabisa alikuwa kwa mikono ya Mungu, lakini kwa sababu ya majaribu ya Shetani na upotovu wake, mwanadamu alifungwa na Shetani na kuanguka katika mikono ya yule mwovu. Kwa hivyo, Shetani akakuwa mlengwa wa kushindwa katika kazi ya Mungu ya usimamizi. Kwa sababu Shetani alichukua umiliki wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu ndiye kiini cha kazi yote ya Mungu ya usimamizi, kama mwanadamu ni wa kuokolewa, basi ni lazima anyakuliwe kutoka mikononi mwa Shetani, ambayo ni kusema kuwa mwanadamu ni lazima achukuliwe baada ya kuwa katika mateka ya Shetani. Shetani anashindwa kupitia mabadiliko ya tabia ya mwanadamu ya zamani ambayo hurejesha hisia zake za awali, na kwa njia hii, mwanadamu, ambaye amechukuliwa mateka, anaweza kunyakuliwa kutoka mikononi mwa Shetani. Kama mwanadamu anawekwa huru kutokana na ushawishi wa Shetani na utumwa wake, Shetani ataaibika, mwanadamu hatimaye atarejeshwa, na Shetani atakuwa ameshindwa. Na kwa sababu mwanadamu ameachiliwa kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani, mwanadamu atakuwa mabaki ya vita hivi vyote, na Shetani atakuwa ndiye mlengwa ambaye ataadhibiwa punde tu vita hivi vitakapokamilika, baada ya kuwa kazi nzima ya wokovu wa mwanadamu itakuwa imekamilika.
kutoka kwa “Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni