8/15/2018

Swahili Christian Movie | Nyendo za Mateso ya Kidini | "Kukaribia Hatari na Kurudi"


Kukaribia Hatari na Kurudi

Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani.
Filamu hii ni masimulizi ya uzoefu wa kweli wa mateso katika mikono ya Chama Cha Kikomunisti cha China yaliyopitiwa na Chen Wenzhong, Mkristo wa Kichina. Chen Wenzhong alikuwa na mafanikio katika kazi yake na alikuwa na familia nzuri na yenye furaha, lakini kwa sababu alimwamini Mungu na kutekeleza wajibu wake, akawa mtu aliyetakiwa na CCP. Alilazimika kuondoka nyumbani na alikuwa mkimbizi kwa zaidi ya miaka kumi. Ili kupata habari za mahali alikokuwa, polisi wa CCP daima waliifuatia, kuitishia, na kuiogofya familia yake, na hata hawangemhurumia mwanawe mdogo wa kiume, Xiaoyu. Hatimaye, walimlazimisha Xiaoyu kutenda kitendo ambacho hangekiepuka …

Kujua zaidi: Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni