8/13/2018

Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Nane

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, ukweli

Kufuatana na sifa za asili za wanadamu, yaani, uso halisi wa wanadamu, kuweza kuendelea hadi sasa hakujakuwa jambo rahisi kweli, na ni kwa njia hii tu ndio nguvu kuu ya Mungu imekuwa dhahiri. Kutegemea kiini cha mwili pamoja na upotovu wa joka kuu jekundu hadi sasa, isingekuwa uongozi wa Roho wa Mungu, mwanadamu angewezaje kusimama leo? Mwanadamu hastahili kuja mbele ya Mungu, lakini Anawapenda wanadamu kwa ajili ya usimamizi Wake na ili kazi Yake kuu iweze kufanikishwa kabla ya muda mrefu sana. Kwa kweli, hakuna mtu anayeweza kulipa upendo wa Mungu kwa wanadamu katika maisha yao yote. Labda wengine wanataka kulipa neema ya Mungu kwa kuyatoa maisha yao, lakini Nakwambia: Mwanadamu hastahili kufa mbele ya Mungu, na kwa hiyo kifo cha mwanadamu ni bure. Kwa sababu kwa Mungu kifo cha mwanadamu hakistahili hata kutajwa, wala hakina thamani ya senti moja, na ni kama kifo cha chungu duniani. Ninashauri watu msijifikiri kuwa wenye thamani sana, na msifikirie kuwa kufa kwa ajili ya Mungu kunabeba uzito wa mlima mkubwa. Kwa Kweli, kifo cha mwanadamu ni suala jepesi kama unyoya. Hakistahili kutambuliwa. Lakini tena, mwili wa mwanadamu umeandikiwa kufa kwa asili, na hivyo mwishoni, maumbile ya mwili yanapaswa kuishia duniani. Huu ni ukweli mwaminifu, na hakuna anayeweza kuukanusha. Hii ni "sheria ya asili" ambayo imejumlishwa kutokana na uzoefu wote wa maisha ya binadamu na Mimi. Na kwa hiyo bila kujua, mwisho wa Mungu kwa mwanadamu huelezwa hivyo. Je, unaelewa? Si ajabu Mungu anasema "Ninadharau uasi wa wanadamu. Sijui kwa nini. Inaonekana Nimemchukia mwanadamu tangu mwanzo, na bado Ninahisi huruma kubwa kwake. Na kwa hiyo mwanadamu ananiangalia kwa mioyo miwili, kwa kuwa Nampenda mwanadamu, na pia Namchukia mwanadamu. "
Nani asiyemtukuza Mungu kwa kuwepo Kwake au kuonekana Kwake? Kwa wakati huu, ni kama kwamba Nimesahau kabisa uchafu na udhalimu ndani ya mwanadamu. Kujidai kwa wanadamu, kujikweza, kutotii, kutojali, na uasi wake wote—Nayasukuma haya yote nyuma ya mawazo Yangu ili kuyasahau. Mungu hazuiliwi kwa sababu ya nafsi kama hiyo ya wanadamu. Kwa kuwa Mungu na Mimi "tunashiriki mateso haya haya," nami pia Nitajiondoa kwenye fumbo hili ili Nisizuiliwe zaidi na mwanadamu. Kwa nini ujisumbue na hilo? Kwa kuwa mwanadamu hayuko radhi kujiunga na nyumba ya Mungu pamoja nami, Nitawezaje kutumia nguvu Zangu kuwakomesha? Sifanyi mambo kulazimisha nguvu Zangu kwao, na si ajabu, kwa sababu Nilizaliwa katika jamii ya Mungu, bila shaka mwanadamu na Mimi daima ni tofauti. Hili limesababisha kushindwa mno kwa leo. Lakini Naendelea kuepukana na udhaifu wa mwanadamu; Nina chaguo gani? Nastahili lawama kwa kutokuwa na nguvu. Si ajabu Mungu anataka "kustaafu" kutoka katika "wakala" wa wanadamu, na anataka "pensheni" Yake. Nanena kutokana na mtazamo wa mwanadamu, na mwanadamu hasikilizi, lakini Ninenapo kama Mungu, je, bado haasi? Labda siku itakuja ambapo Mungu kwa kweli “atastaafu” ghafla kutoka katika "wakala" wa wanadamu, na wakati huo utakapokuja, neno la Mungu litakuwa kali zaidi. Leo, inaweza kuwa kwa sababu Yangu ndio Mungu ananena hivi, na siku hiyo ikija, Mungu hatakuwa tena kama Mimi, kwa subira "akiwatambia watoto hadithi katika shule ya chekechea." Labda kile Nisemacho hakigongi ndipo. Ni kwa ajili ya Mungu mwenye mwili tu ndio Mungu yuko radhi kulegeza mshiko Wake kwa mwanadamu kidogo, la sivyo, ingekuwa ya kutisha sana kutafakari. Kama vile Mungu alisema, “Nililegeza fumbato Langu kwao kwa kiasi fulani, kuwaruhusu kujiingiza katika tamaa zao za mwili, na hivyo walithubutu kuwa jeuri, bila kizuizi, na inaweza kuonekana kuwa hawakunipenda kweli, kwa vile waliishi katika mwili.” Kwa nini Mungu anasema hapa "kujiingiza katika tamaa zao," na "waliishi katika mwili"? Kwa kweli, maneno haya hayahitaji ufafanuzi Wangu, na yanaweza kueleweka kwa kawaida. Labda watu wengine wanasema hawaelewi, lakini Nitakwambia kuwa unajua ukweli, na unajifanya tu hujui. Nakukumbusha: Kwa nini Mungu anasema “Mimi Namwomba mwanadamu kushirikiana Nami tu"? Kwa nini Mungu anasema kuwa asili ya binadamu ni ngumu kubadilika? Kwa nini Mungu hudharau asili ya binadamu? Na asili ya mwanadamu ni nini hasa? Asili ya mwanadamu si nini? Nani amezingatia maswali haya? Pengine hii ni mada mpya kwa mwanadamu, lakini haijalishi, Namwomba mwanadamu aifikirie sana, la sivyo utamchukiza Mungu daima kwa sababu ya maneno kama "asili ya binadamu haiwezi kubadilika." Kuna maana gani katika kutenda kinyume Chake kwa njia hiyo? Je, huko si kutafuta shida? Je, mwishowe, si kama tu kurusha yai dhidi ya jiwe?
Kwa kweli, majaribio na majaribu yote yanayomjia mwanadamu ni masomo ambayo Mungu anahitaji kwa mwanadamu. Kufuatana na nia ya asili ya Mungu, hata kama mwanadamu atakuwa tayari kutengana na kitu anachopenda, bado linaweza kutimizwa. Tatizo ni kuwa mwanadamu daima anajipenda tu, kwa hiyo anashindwa kushirikiana kweli na Mungu. Mungu hataki mengi kutoka kwa mwanadamu. Yote ambayo Mungu anataka kwa mwanadamu yanahitaji kutimizwa kwa urahisi na kwa furaha; ni vile tu mwanadamu hayuko radhi kupitia shida. Kama watoto, angeweza kuishi kwa uangalifu ili kupata senti chache kuwaheshimu wazazi wake na kutimiza wajibu anaopaswa kutimiza. Lakini anaogopa kwamba hatakula vizuri vya kutosha na kwamba mavazi yake yatakuwa ya kawaida sana, kwa hiyo kwa sababu moja au nyingine, anachukua upendo na utunzaji wa wazazi wake na kuvitupa mbali sana katika mawingu, kama kwamba ataanza kufanya hili baada ya kupata kiasi kikubwa cha fedha. Lakini Naweza kuona kutokana na hili kwamba wanadamu hawana utiifu wa mapenzi wa kuwapenda wazazi wao—ni wana wasio na mapenzi kwa wazazi. Pengine hili ni kali mno, lakini Siwezi kufoka upuuzi kinyume na ukweli. Siwezi “kuwaiga wengine” ili kumpinga Mungu kwa kujiridhisha Mwenyewe. Ni kwa sababu hakuna mtu hapa duniani aliye na upendo wa watoto kwa wazazi ndio Mungu alisema: “Mbinguni, Shetani ni adui Yangu, duniani, mwanadamu ni adui Yangu. Kwa sababu ya muungano kati ya mbingu na dunia, vizazi tisa vyao vinapaswa kuchukuliwa kuwa na hatia kwa ushirikiano.” Shetani ni adui wa Mungu; sababu Ninayosema hiyo ni kwa sababu hamlipi Mungu kwa neema na fadhili Zake, lakini badala yake "hupiga kasia kinyume na mkondo," na kwa kufanya hivyo hatimizi "utiifu wa kuwapenda wazazi" kwa Mungu. Je, watu hawako hivi pia? Hawaonyeshi heshima ya upendo kwa “wazazi” wao na hawalipi malezi na msaada wa "wazazi" wao. Hili linatosha kuonyesha kwamba watu wa dunia ni jamaa ya Shetani mbinguni. Mwanadamu na Shetani ni wa moyo mmoja na akili moja dhidi ya Mungu, na kwa hiyo si ajabu Mungu anahusisha vizazi tisa kama wenye hatia kwa ushirikiano na hakuna anayeweza kusamehewa. Katika siku za nyuma, Mungu alikuwa na mtumishi mnyenyekevu mbinguni ambaye Alimuita kusimamia wanadamu, lakini hakusikia, na akafanya kulingana na silika yake ya kuasi dhidi Yake. Je, si wanadamu waasi pia wanapiga hatua mbele kwenye njia hii? Haijalishi ni kiasi gani Mungu anakaza "hatamu," watu hawatikisiki kamwe tu na hawawezi kugeuka. Kwa maoni yangu, kama mwanadamu ataendelea kwa njia hii, ataharibiwa, na labda ni wakati huu ndio utaelewa maana halisi ya maneno haya: "mwanadamu hawezi kujifundua kwa asili yake ya kale?” Mungu amemkumbusha mwanadamu mara nyingi: "Kwa sababu ya uasi wa mwanadamu, Nimemwacha." Kwa nini Mungu anasema hivi tena na tena? Je, Mungu anaweza kuwa katili hivyo? Kwa nini Mungu anasema pia "Mimi si mwanadamu hasa"? Kwa siku nyingi zilizotulia, ni nani ambaye amechunguza kweli masuala haya kwa kina? Nawahimiza wanadamu waweke juhudi zaidi katika maneno ya Mungu na wasiyachukulie kwa wepesi; hili halina faida kwako, au kwa wengine. Ni vyema kutosema kile ambacho hakihitajiki kusemwa, na kutofikiri juu ya kile ambacho hakihitajiki kuzingatiwa. Je, hilo si rahisi zaidi? Je, ni kosa gani linaweza kutokana na hili? Kabla ya Mungu kutangaza mwisho wa kazi Yake duniani, hakuna mtu ataacha "kusonga"; hakuna mtu atakayejitoa kabisa katika wajibu wake. Sasa sio wakati; usijifanye kuwa kiongozi kwa Mungu, au mtangulizi. Nadhani ni mapema sana kukoma sasa na kuacha kusonga mbele—unaonaje?
Mungu humleta mwanadamu katika kuadibu, na Huwaingiza katika mazingira ya kifo, lakini kwa upande mwingine, ni nini ambacho Mungu anataka mwanadamu afanye duniani? Kujifanya kama kabati la nguo nyumbani? Haliwezi kuliwa au kuvaliwa, bali kutazamwa tu. Ikiwa ni hivyo, kwa nini utumie michakato mingi migumu, kuwafanya watu wateseke sana katika mwili? Mungu Asema, “Namsindikiza kwenye ‘uwanja wa kuua,’ kwa kuwa hatia ya wanadamu inatosha kustahili kuadibu Kwangu.” Kwa wakati huu, je, Mungu anawafanya watu watembee kwenda kwa uwanja ya kuua wenyewe? Kwa nini hakuna mtu anayewaombea msamaha? Basi, mwanadamu anapaswa kushirikiana jinsi gani? Je, mwanadamu anaweza kufanya mambo kweli bila kuathiriwa na hisia, kama Mungu Anavyofanya hukumu Zake? Ufanisi wa maneno haya hasa unategemea matendo ya mwanadamu. Kama baba anavyopata pesa, ikiwa baadaye mama hajui jinsi ya kushirikiana, bila kujua jinsi ya kusimamia nyumba, basi nyumba hiyo itakuwa katika hali gani? Angalia hali ya kanisa sasa; Je, nyinyi kama viongozi mtafikiria nini? Nyinyi mnaweza kuwa na mkutano ambapo kila mtu anaweza kuzungumza kuhusu fikira zao kibinafsi. Mama hufanya machafuko ya vitu nyumbani, kwa hiyo watoto wa familia hii watakuwa kama nani? Mayatima? Waombaji? Si ajabu Mungu alisema: "Watu wote wanadhani kwamba Mimi ni uungu unaokosa "ubora wa akili," lakini ni nani anayeweza kuelewa kwamba Naweza kubaini kila kitu katika ubinadamu?" Kuhusu hali dhahiri kama hiyo, hakuna haja ya kuzungumza kutoka kwa uungu Wake. Kama alivyosema Mungu, "hakuna haja ya kugonga msumari kwa nyundo kubwa." Kwa wakati huu, labda kuna watu wengine ambao wana uzoefu wa vitendo na neno la Mungu la hekima: "Miongoni mwa wanadamu, hakuna yeyote anayenipenda." Wakati huu, ni vile tu alivyosema Mungu: "Watu wote wanainamisha vichwa vyao kwa kusita kwa sababu ya hali ya sasa, lakini mioyo yao bado haijaridhika." Maneno haya ni kama darubini. Katika siku za karibu za usoni, mwanadamu ataingia katika hali nyingine. Hii inaitwa kutorekebishika. Je, mnaelewa? Hilo ndilo jibu kwa maswali haya mawili ya Mungu: "Je, watu hawaepuki dhambi tu kwa sababu wanaogopa Nitaondoka? Je, si kweli kwamba hawalalamiki tu kwa sababu wanaogopa kuadibu?" Kwa kweli, sasa watu ni wazembe kidogo na wanaonekana wamechoka sana, na hawajali kabisa kutilia maanani kazi ya Mungu, na wanajishughulisha tu na utaratibu na mipango ya miili yao. Je, huu si ukweli?

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni