7/21/2018

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Kwanza

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli

Kama tu Mungu alivyosema, “Hakuna anayeweza kuelewa mzizi wa maneno Yangu, wala kusudi la maneno haya.” Kama Isingekuwa uongozi wa Roho wa Mungu, kama isingekuwa kwa majilio ya maneno Yake, wote wangeangamia chini ya kuadibu Kwake. Ni kwa nini Mungu humjaribu mwanadamu kwa muda mrefu hivyo? Na kwa muda mrefu kama miezi mitano? Hili ndilo wazo la kulenga la ushirika wetu na vilevile wazo kuu katika hekima ya Mungu.  Tunaweza kuchukulia kwamba: Isingekuwa jaribio hili, na bila Mungu kushambulia, kuua, na kuwatema binadamu wapotovu, ikiwa ujenzi wa kanisa ungeendelea mpaka leo, basi hilo lingefanikisha nini? Kwa hiyo katika mstari wa kwanza wa hotuba Yake, Mungu anaenda moja kwa moja kwa wazo hilo na kueleza athari inayotakiwa ya kazi ya miezi hii, na ni sahihi kabisa! Inaelekea kuonyesha hekima ya matendo ya Mungu katika kipindi hiki cha wakati: kuwafunza watu kujifunza utii na kujitolea kwa uaminifu kupitia majaribio, na vilevile jinsi ya kumfahamu Mungu bora kupitia usafishaji wa uchungu. Kadri watu wanavyopitia kukata tamaa, ndivyo wanavyoweza kujifahamu wenyewe. Na kusema kweli, kadri wanavyopitia usafishaji wa uchungu, ndivyo wanavyoweza kufahamu zaidi upotovu wao wenyewe, na kwa kufanya hivyo hata wanajifunza kwamba hawastahili kuwa “mtendaji-huduma” wa Mungu, na kufanya aina hii ya huduma ni kuinuliwa na Yeye. Na kwa hiyo mara tu hili linapotimizwa, mara tu mwanadamu anapojipunguza mwenyewe, Mungu hutamka maneno ya huruma, sio yaliyofichwa bali yanayoonekana wazi. Ni wazi kwamba baada ya miezi kadhaa, njia mpya[a] ya kazi ya Mungu inaanza leo; hili ni wazi kwa wote kuona. Katika wakati uliopita, Mungu alisema mara kwa mara “si rahisi kustahili haki ya kuitwa watu Wangu,” kwa hiyo kama Alivyotimiza maneno haya ndani ya watu wanaotajwa kama watendaji huduma, wote huenda wakaona kwamba Mungu anaweza kuaminiwa bila kosa lolote. Yote ambayo Mungu husema yatakuwa kweli kwa viwango tofautitofauti, na maneno Yake sio matupu hata kidogo.
Wanadamu wote wanapokuwa wenye kuhangaika na wa kusikitishwa, maneno haya kutoka kwa Mungu huwa na maana kwa wote wanaojikuta hawana matumaini, na huwahuisha wao. Ili kuondoa shaka zaidi, Mungu aliongeza kwamba “ingawa hili jina la watu Wangu, wao kamwe si wa hadhi ya chini kuitwa ‘wana’ Wangu.” Hapa mtu anaweza kuona kwamba Mungu pekee ndiye anaweza kuhifadhi mamlaka Yake, na watu wakishayasoma wanaamini thabiti zaidi kwamba hii sio njia ya kufanya kazi, bali ukweli. Zaidi ya hayo, ili maono ya watu yasiwe yenye giza, katika njia Yake mpya utambulisho wa watu wote unakuwa wazi zaidi. Kutokana na hili, mtu anaweza kuona hekima ya Mungu. Hivi watu wanaweza kufahamu bora kwamba Mungu anaweza kuona ndani kabisa ya mioyo ya wanadamu; kama vile makaragosi, yote wanayofanya na yote wanayofikiria yanaendeshwa na Mungu. Hili ni thabiti.
Tukirudi mwanzo, kile Mungu alisema kwanza ni kwamba hatua ya kwanza ya kazi Yake, “kulitakasa kanisa,” ishakamilishwa. “Hali sio kama ilivyokuwa wakati fulani, na kazi Yangu imeingia katika kiwango kipya cha kuanza.” Kutokana na kauli hii, mtu anaweza kuona kwamba kazi ya Mungu imeingia katika kiwango kipya cha kuanza, na punde baada ya Yeye kutaja mpango makini wa hatua inayofuata ya kazi Yake kwetu—baada ya kumaliza ujenzi wa kanisa, maisha ya Enzi ya Ufalme yataanza. “kwani sasa sio enzi ya kujenga kanisa tena, lakini badala yake ni enzi ambamo ufalme unajengwa kwa ufanisi.” Kuongezea, Ameonyesha kwamba kwa vile watu bado wako duniani, makusanyiko yao yataendelea kutajwa kama kanisa, na kwa njia hii utambuzi usio halisi wa “ufalme” wa mawazo ya watu unaepukwa. Kinachofuata, Nitakuwa na ushirika juu ya suala la maono.
Sasa ni enzi ya ujenzi wa ufalme na mwisho wa ujenzi wa kanisa; ilhali, ni kwa nini makusanyiko yote bado yataitwa kanisa? Hapo awali kanisa lilitajwa kama utangulizi wa ufalme; bila kanisa hakungekuwa na ufalme. Enzi ya Ufalme inaanza na Mungu akitekeleza huduma Yake katika mwili, na Enzi ya Ufalme inaletwa na Mungu mwenye mwili. Anacholeta ni Enzi ya Ufalme, sio majilio rasmi ya ufalme. Hili si gumu kuwaza; watu wanaozungumziwa ni watu wa Enzi ya Ufalme, sio watu wa ufalme wenyewe. Hivyo, inaeleweka kwamba makusanyiko duniani bado yangetajwa kama kanisa. Hapo zamani, Alitenda kupitia kwa ubinadamu Wake wa kawaida, na hakushuhudiwa kama Mungu Mwenyewe, hivyo Enzi ya Ufalme haikuwa imeanza miongoni mwa wanadamu; yaani, kama Nilivyosema, Roho Wangu hakuwa ameanza kufanya kazi rasmi ndani ya umbo Langu lenye mwili. Kwa vile sasa Mungu Mwenyewe ameshuhudiwa, ufalme umetambuliwa miongoni mwa wanadamu. Hili linaashiria kwamba Nitaanza kufanya kazi kupitia kwa uungu, na hivyo wale wanaoweza kukubali maneno Yangu na matendo Yangu katika uungu wanajulikana kama watu Wangu wa Enzi ya Ufalme, na hivi ndivyo neno “watu Wangu” linatokea. Katika hatua hii, kimsingi Nafanya kazi na kuzungumza kupitia kwa uungu Wangu. Mwanadamu hawezi kuingilia, wala kuweza kuvuruga mpango Wangu. Mara tu neno la Mungu lifikapo kiwango fulani, jina Lake hushuhudiwa, na majaribio Yake ya wanadamu huanza. Huu ni mfano mkuu zaidi wa hekima ya Mungu. Hili linaweka msingi imara na kukita mizizi kwa ajili ya kuanza hatua inayofuata na vilevile hitimisho la hatua ya mwisho. Mwanadamu hakuwa na njia ya kulijua hilo; hiki ndicho kiwango cha kukutana cha sehemu ya kwanza na ya pili ya enzi ya hukumu. Bila miezi michache ya usafishaji wa mwanadamu, Sikuweza kufanya kazi kupitia uungu Wangu. Hii miezi ya usafishaji hufungua njia ya hatua inayofuta ya kazi Yangu. Mwisho wa kazi hii ya miezi michache ni ishara ya kuingia ndani zaidi katika awamu inayofuata ya kazi. Ikiwa mtu kweli anaelewa maneno ya Mungu, mtu huenda akaelewa kwamba Anatumia miezi hii kuanza hatua inayofuata ya kazi Yake ili iweze kuzaa matunda zaidi. Kipingamizi cha ubinadamu Wangu kimesababisha kizuizi kwa ngazi inayofuata ya kazi Yangu, kwa hiyo kupitia hii miezi ya usafishaji wa uchungu, pande zote mbili zinaadilishwa na kunufaika kutokana na hilo. Ni sasa tu ndio mwanadamu huanza kuthamini mtindo Wangu wa kuhutubu. Na kwa hiyo kwa mgeuzo wa kalamu Yake, Mungu aliposema Hatamwita tena mwanadamu “mtendaji-huduma,” lakini badala yake “watu Wake,” wote walijawa na furaha. Huu ulikuwa udhaifu wa mwanadamu. Mungu alikuwa ameuteka.

Ili kuwaridhisha zaidi wanadamu wote na kuonyesha najisi ndani ya ibada ya watu wengine, Mungu ameenda mbele zaidi kuonyesha sehemu mbalimbali zisizovutia za wanadamu, na kwa njia hii Ametimiza maneno Yake kama yafuatayo: “Ni wangapi wananipenda Mimi kweli? Ni nani asiyetenda kwa kuzingatia siku zake mwenyewe za baadaye? Ni nani hajawahi kulalamika wakati wa majaribio yake?” Kutokana na maneno haya, wanadamu wanaweza kuona kutotii kwao wenyewe, kutokuwa waaminifu na ukosefu wa utiifu kwa mzazi, na hivyo kuona huruma na upendo wa Mungu vikiwafuata wote wanaomtafuta Yeye katika kila hatua ya njia. Hili linaweza kuonekana kutokana na na maneno haya: “Sehemu ya mwanadamu inapokuwa karibu kabisa kurudi nyuma, wakati wote wanaonitarajia Mimi kubadilisha mtindo Wangu wa kuhutubu wanakosa tumaini, Ninatamka maneno ya wokovu, na kuwarudisha wote wanipendao Mimi kweli kwa ufalme Wangu, mbele ya kiti Changu cha enzi.” Hapa, kirai “wale wanipendao Mimi kweli,” na swali la balagha “Ni wangapi wanipendao Mimi kweli?” havipingani. Inaonyesha kwamba wale ambao ni wa kweli wana najisi. Sio kama kuwa Mungu hajui chochote. Kwa vile Mungu anaweza kuona sehemu ya ndani zaidi ya mioyo ya wanadamu, neno “kweli” linatumiwa kwa stihizai kwa kurejelea upotovu wa wanadamu, ili wanadamu wote waweze kuona vizuri kuwa kwao wadeni wa Mungu, wachukue lawama zaidi, na vilevile kuelewa kweli kwamba chuki iliyo ndani ya mioyo yao yote inatoka kwa Shetani. Watu hushangaa wanapoona neno “ibada.” Wao hufikiri: Ni mara ngapi nimekosoa Mbingu na dunia? Na ni mara ngapi nimetaka kuondoka, lakini kwa vile niliogopa amri za usimamizi za Mungu nilivumilia tu na kushirikiana na umati, kumngoja Mungu alitatue? Ikiwa ingedhihirika kwamba hakukuwa na tumaini kwa hakika, basi ningejiondoa polepole. Sasa Mungu anatuita watu Wake waliojitolea, kwa hiyo hii inamaanisha kwamba Mungu kwa kweli anaweza kuona moja kwa moja ndani ya sehemu ya ndani kabisa ya mioyo ya wanadamu? Ni mpaka mwisho kabisa ndipo Mungu alionyesha hali za ndani za aina mbalimbali ya watu ili kuepuka aina hii ya suitafahamu. Hili liliwafanya wanadamu ambao hapo mwanzo walikuwa wenye shaka ndani ya mioyo yao lakini wenye furaha katika maneno yao kuingia katika hali ya kuondoa shaka ndani ya moyo, maneno, na macho. Kwa njia hii, fikira za mwanadamu za maneno ya Mungu zimekuwa kubwa zaidi, na kulingana na hilo mwanadamu amekuwa na woga zaidi, uchaji zaidi, na amepata ufahamu bora zaidi wa Mungu. Hatimaye, ili kupunguza woga wa mwanadamu wa siku za baadaye, Mungu alisema: “Lakini kwa vile siku zilizopita ni siku zilizopita, na sasa ni wakati uliopo, hakuna haja ya kutamani tena siku zilizopita, au kuwa na wasiwasi kuhusu siku za usoni.” Aina hii ya njia ya kuzungumza ya haraka, patanifu, ilhali ya mkato ina hata athari kubwa zaidi, ikiwaruhusu wote wanaoyasoma maneno Yake kuiona nuru mara nyingine katika kufa moyo kwao, halafu waone hekima na matendo ya Mungu, kisha wapate jina la heshima la “watu wa Mungu,” na baada ya hapo waondoe shaka iliyo ndani ya mioyo yao, na kisha wajifunze kujijua wenyewe kutokana na hali zao mbalimbali za ndani. Hali hizi huonekana katika zamu, simanzi pamoja na huzuni, na furaha na shangwe. Mungu ameteka muhtasari wa mfano wa maisha wa watu katika maneno haya. Ni dhahiri kwa kiwango cha ukamilifu, kitu ambacho mwanadamu hawezi kutimiza. Inafichua kwa kweli siri zilizo ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu. Je, hili ni jambo ambalo mwanadamu angefanya?
Hata muhimu zaidi ni fungu la maneno lililo hapa chini, ambamo Mungu anafichua kwa mwanadamu moja kwa moja amri Yake ya usimamizi. Na hii ndiyo sehemu muhimu zaidi: “Miongoni mwa wanadamu, wale wanaoenda kinyume cha uhalisi na hawafanyi mambo kulingana na uongozi Wangu hawatakuwa na mwisho mzuri, na watajiletea tu matatizo. Kwa kila kitu kinachotokea ulimwenguni, hakuna kitu Nisichokuwa na usemi wa mwisho kukihusu.” Je, hii sio amri ya usimamizi ya Mungu? Inaelekea kuonyesha kwamba kuna mifano mingi ya wale ambao hutenda dhidi ya amri hii ya usimamizi. Zaidi ya hayo, inamwonya kila mtu asifikirie juu ya kudura yake mwenyewe. Ikiwa mtu anataka kuutoroka mpango wa Mungu, matokeo yatakuwa ya kutisha yapitayo mawazo. Hivyo, inawafanya wale wote wanaopitia kupata nuru na mwangaza katika maneno haya waweze kuelewa bora zaidi amri ya usimamizi za Mungu na vilevile kuelewa kwamba uadhama Wake usikosewe, na hivyo kuwa wenye uzoefu zaidi na watulivu na waliomakinika, wa kijani kibichi kama msonobari uliopona ambao umekiuka vitisho vya baridi kali, unaoendelea kuongeza kwa uzima wa kijani kibichi kinachostawi cha asili. Kauli hii huwafanya watu wengi wahisi kukanganyikiwa kisulisuli, kana kwamba wamepotelea katika aina fulani ya mzingile; hili ni kwa sababu maudhui ya maneno ya Mungu hubadilika upesi kiasi, kwa hiyo watu tisa kutoka kwa kumi huingia katika matata mengi wanapojaribu kufahamu tabia zao wenyewe za upotovu. Kwa ajili ya kufanya kazi kwa urahisi, kuondoa shaka ya mwanadamu, na ili wote waweze kuamini zaidi katika uaminifu wa Mungu, Anasisitiza mwisho wa kifungu hicho cha maneno: “Kila mmoja wa wale wanaonipenda kweli watarudi mbele ya kiti Changu cha enzi.” Hivyo, wale wote ambao wamepitia miezi mingi ya kazi Yake wanapunguziwa huzuni yao mara moja; mioyo yao, ambayo ilihisi kana kwamba imening'inizwa katikati ya hewa, hurudi nyumbani kama jiwe linaloanguka kwa ardhi ngumu; huwa hawana wasiwasi tena kuhusu majaliwa yao, hawaamini tena kwamba Mungu atazungumza maneno matupu. Kwa vile wanadamu ni wa kujidai, hakuna hata mmoja asiyeamini kwamba anaonyesha kujitolea kwa juu sana kwa Mungu; hii ndio maana kwa makusudi Mungu anasisitiza “kweli”—ni kutimiza matokeo makuu zaidi. Hii ni njia na kuweka msingi wa hatua inayofuata katika kazi Yake. 
Tanbihi:
a. Maandishi ya asili yanaacha “mpya.”

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni