7/06/2018

Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, upendo wa Mungu

Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu

Kwa mwanadamu, haiwezekani kwa wana wa Moabu kuwa wakamilifu na hawajahitimu kufanywa hivyo. Wana wa Daudi, kwa upande mwingine, hakika wana matumaini na hakika wanaweza kufanywa kamili. Kwa sharti kwamba mtu ni mzawa wa Moabu, basi hawezi kufanywa kamili. Hata leo, bado hamjui umuhimu wa kazi inayofanyika miongoni mwenu; mpaka katika hatua hii ya sasa bado mnashikilia matumaini yenu ya baadaye katika mioyo yenu na hamtaki kuyaacha. Hakuna mtu anayejali ni kwa nini leo Mungu amewachagua tu—kikundi kisichostahili mno—kukifanyia kazi, hivyo je, kazi hii inafanywa vibaya? Je, hii ni kazi ya uangalizi wa muda mfupi? Kwa nini Mungu ameshuka chini bila upendeleo kufanya kazi kati yenu, ingawaje Amekuwa akijua kwa muda mrefu kwamba nyinyi ni wana wa Moabu? Je, hamfikiri kuhusu jambo hili asilani? Je, Mungu hafikirii kamwe juu ya hili Anapofanya kazi Yake? Je, Yeye hufanya uamuzi wa aina hii wa upesi upesi? Je, Hakujua kwamba ninyi ni wana wa Moabu tangu mwanzo? Je, hamjui kuzingatia mambo haya? Je, "dhana" zenu zimekwenda wapi? Je, mawazo yenu maridhawa yamerekebishwa visivyo? Je, ustadi wenu na hekima yenu zimekwenda wapi? Je, ni kwamba mna ujeuri kama huu wa ajabu ndiyo hamjali jambo kama hilo? Mawazo yenu yana wepesi sana wa kuona kwa mambo kama matarajio yenu ya baadaye na hatima yenu wenyewe, lakini juu ya chochote kingine hayajali na ni yenye upumbavu na ujinga kabisa. Ni nini sasa mnayoamini? Matumaini yenu ya baadaye? Au Mungu? Je, si wewe unaamini tu hatima yako nzuri? Matarajio yako ya baadaye tu? Je, unaelewa kiasi kipi kuhusu njia ya maisha? Je, umefikia kiasi gani? Je! unafikiri kwamba kazi inayofanyika sasa juu ya wana wa Moabu inafanywa ili kukufedhehesha? Je, inafanywa kimakusudi ili kufichua ubaya wenu? Je, inafanywa kimakusudi ili kuwafanya ninyi kukubali kuadibu na kisha kuwatupa katika ziwa la moto? Sijawahi kusema kuwa hamkuwa na mategemeo, sembuse kwamba mlipaswa kuangamizwa au kupotea; je, Nimetangaza hadharani jambo hilo? Wewe husema kuwa huna tumaini, lakini si hili ni hitimisho lako? Je, si hii ni athari ya mawazo yako mwenyewe? Je, hitimisho lako lina maana? Nikisema wewe hujabarikiwa basi utakuwa kitu cha kuharibiwa, na Nikisema umebarikiwa basi wewe hakika hutaangamizwa. Ninasema sasa tu kwamba wewe ni mzao wa Moabu. Sikusema kuwa wewe utaharibiwa. Ni kwamba tu wana wa Moabu wamelaaniwa, na ni aina moja ya wanadamu waliopotoshwa. Dhambi zimerejelewa awali; Je, si nyinyi nyote ni wenye dhambi? Je, wenye dhambi wote si wamepotoshwa na Shetani? Je, wenye dhambi wote si wanakosa kutii na wanaasi dhidi ya Mungu? Je, wale wanaomdharau Mwenyezi Mungu sio vitu vya laana? Lazima wenye dhambi wote wasiangamizwe? Katika hali hiyo, ni nani kati ya wale wa mwili na damu anayeweza kuokolewa? Mnawezaje kuwa mmeokoka mpaka leo? Ninyi ni wabaya kwa sababu ninyi ni wana wa Moabu, na je, ninyi sio miongoni mwa wenye dhambi wa wanadamu? Je, mmedumu vipi hadi leo? Ukamilifu unapotajwa mnakuwa na furaha. Mmesikia kwamba mnapaswa kupitia shida kubwa, na mnafikiri kuwa hili limebarikiwa hata zaidi. Mnafikiri kuwa kwa njia ya dhiki mnaweza kuwa washindi, na hii ni zaidi ya baraka kubwa ya Mungu na furaha yake kuu kwenu. Moabu anaporejelewa, mshtuko unatokea kati yenu. Watu wazima na watoto pia huhisi huzuni isiyoelezeka na mioyo yenu inajaa dhiki; ninyi nyote mnajuta kuzaliwa. Hamwelewi umuhimu wa kwa nini hatua hii ya kazi inafanywa kwa wana wa Moabu; mnajua tu kutafuta hadhi ya juu, na mnarudi nyuma mnapofikiria kuwa hamna tumaini. Ukamilifu na hatima ya baadaye vinapotajwa, mnahisi furaha. Imani yenu kwa Mungu ni ili kupata baraka, na ili muwe na hatima nzuri. Watu wengine sasa wanahisi wasiwasi kwa sababu ya hadhi zao. Kwa sababu wana thamani ya chini, na hali ya chini, basi hawataki kutafuta kukamilishwa. Mungu kwanza alizungumza juu ya ukamilifu, kisha baadaye Akarejelea wazao wa Moabu, kwa hivyo watu walikana njia ya ukamilifu waliyokuwa wamefuata hapo awali. Hii ni kwa sababu hamjawahi kutambua umuhimu wa kazi hii, wala hamjali juu ya umuhimu wake. Vimo vyenu ni vidogo sana na hamuwezi hata kuvumilia usumbufu kidogo. Mnapoona kwamba hali yenu wenyewe ni duni sana mnahisi hasi, na hamna imani ya kuendelea kutafuta. Watu huona tu kupata neema na furaha ya amani kama ishara ya imani katika Mungu, na kutafuta baraka kama msingi wa imani katika Mungu. Watu wachache sana wanatafuta kumjua Mungu au kutafuta mabadiliko katika tabia zao. Imani ya watu katika Mungu hutafuta kumfanya Mungu kuwapa hatima inayofaa, kuwapa neema yote chini ya jua, kumfanya Mungu mtumishi wao, kumfanya Mungu adumishe uhusiano wa amani, wa kirafiki pamoja nao, na ili kusiwe na mgogoro wowote kati yao. Yaani, imani yao kwa Mungu inahitaji Mungu kutoa ahadi ya kutimiza mahitaji yao yote, kuwapa chochote wanachoomba, kama ambavyo inasema katika Biblia "Nitazisikiliza sala zenu zote." Wanahitaji Mungu kutomhukumu mtu yeyote au kushughulika na mtu yeyote, kwa kuwa Mungu daima ni Mwokozi Yesu mkarimu, ambaye huwa na uhusiano mzuri na watu wakati wote na mahali pote. Wanavyoamini ni hivi: Wao daima humwomba Mungu vitu bila haya, na Mungu huwapa kila kitu kwa upofu, kama wao ni waasi au watiifu. Watu daima wanataka "malipo" kutoka kwa Mungu na Mungu lazima Alipe bila upinzani wowote, na kulipa mara dufu, kama Mungu amepata chochote kutoka kwao au la. Anaweza tu kuwa chini yao; Hawezi kuwapanga watu kiholela, sembuse Hawezi kuwafunulia watu hekima Yake ya kale ya siri na tabia ya haki kama Anavyotaka, bila ruhusa yao. Wao huungama tu dhambi zao kwa Mungu na Mungu huwasamehe tu, na Hawezi kuchoshwa na hilo, na hii inaendelea milele. Wanamwamuru Mungu tu na Yeye anatii tu, kama ilivyonakiliwa katika Biblia ikisema "Kuja kwa Mungu si kumfanya mtu amsubiri, bali ili Yeye amsubiri mwanadamu. Amekuja kumtumikia mwanadamu. " Je, si siku zote mmeamini kwa njia hii? Wakati ambapo hamuwezi kupata chochote kutoka kwa Mungu basi mnataka kukimbia. Na wakati ambapo hamuelewi kitu mnapata hasira, na hata kwenda mbali ili kutoa aina zote za matusi. Hamuwezi tu kumruhusu Mungu Mwenyewe kuonyesha kikamilifu hekima na shani Yake, lakini badala yake unataka tu kufurahia urahisi wa muda na faraja. Hadi sasa, mtazamo wenu katika imani yenu kwa Mungu umekuwa sawa na maoni ya zamani. Mungu akiwaonyesha utukufu mdogo tu mnakosa furaha; je, mnaona sasa jinsi kimo chenu kilivyo? Msifikiri kuwa ninyi nyote ni waaminifu kwa Mungu wakati kwa kweli maoni yenu ya zamani hayajabadilika. Wakati ambapo hakuna chochote kibaya kinachokuangukia, unafikiri kwamba kila kitu kinaelekea kwa urahisi na unampenda Mungu kwa vilele vya juu zaidi. Lakini kitu kidogo kinapokukumba, unakushuka kuzimuni. Je, hii ni wewe kuwa mwaminifu kwa Mungu?
Kama hatua ya mwisho ya kazi ya ushindi ingeanzia Israeli, basi kazi ya ushindi isingekuwa na maana. Kazi ni ya umuhimu zaidi wakati ikiwa inafanyika nchini humu, inapofanyika kwenu enyi watu. Ninyi ni watu wanyenyekevu zaidi, watu walio na hadhi ndogo zaidi. Ninyi ni watu katika ngazi ya chini kabisa ya jamii hii na ninyi ndio ambao walimtambua Mungu kwa kiwango cha chini sana mwanzoni . Ninyi ni watu ambao wamekwenda mbali zaidi na Mungu, na ni wale ambao wamejeruhiwa vibaya. Kwa sababu hatua hii ya kazi ni kwa ajili tu ya ushindi, je, haifai zaidi kuwachagua kuwa na ushuhuda ujao? Ikiwa hatua ya kwanza ya kazi ya ushindi haikufanyika kwenu, basi itakuwa vigumu kuendeleza kazi ya kushinda inayokuja, kwa sababu kazi ya ushindi ambayo itafuatia itafikia matokeo kulingana na ukweli kuwa hii Kazi inafanyika leo. Kazi ya ushindi leo ni mwanzo tu wa kazi nzima ya ushindi. Ninyi ni kundi la kwanza kushindwa; ninyi ni wawakilishi wa wanadamu wote ambao wanashindwa. Ikiwa kuna mtu yeyote aliye na ufahamu kweli, ataona kwamba kazi yote ambayo Mungu anafanya leo ni kubwa, kwamba Mungu hawaruhusu tu watu kujua uasi wao wenyewe, Yeye pia hufunua hali zenu. Madhumuni na maana ya maneno Yake sio kuwafanya watu kuwa wabaya, wala sio kusababisha watu kuanguka chini. Ni ili kwamba waweze kupata ufunuo na kuokolewa kupitia maneno Yake; ni kufufua roho ya mwanadamu kupitia maneno Yake. Kutoka wakati wa uumbaji wa dunia mpaka sasa, mwanadamu daima ameishi chini ya utawala wa Shetani, bila kujua kwamba kuna Mungu na kutoamini kuna Mungu. Kwamba watu hawa wanaweza kuingizwa katika wokovu mkuu wa Mungu na kuinuliwa sana na Mungu kwa kweli inaonyesha upendo wa Mungu; wale wanaoelewa kweli wote watafikiria kwa njia hii. Je, watu hao wasio na ufahamu watafikiria vipi? "Ah, Mungu anasema sisi ni uzao wa Moabu. Alisema Mwenyewe kuwa sisi ni wana wa Moabu. Je, tunaweza kuwa wazuri? Ni nani aliyetufanya sisi kuwa wana wa Moabu? Ni nani ambaye alitufanya hapo awali kumuasi Yeye sana? Mungu amekuja kutuhukumu; je, huoni jinsi Mungu alivyotuhukumu daima tangu mwanzo? Kwa kuwa tumemkataa Mungu tunapaswa kuadibiwa kwa njia hii.” "Je, maneno haya ni sahihi? Leo Mungu anawahukumu, na kuwaadibu, na kuwashutumu, lakini jueni kwamba shutuma yako ni ili kukufanya kuweza kujijua. Shutuma, laana, hukumu, kuadibu—haya yote ni ili kwamba uweze kujijua, ili tabia yako iweze kubadilika, na, zaidi ya hayo, ili uweze kujua thamani yako, na kutambua kwamba vitendo vyote vya Mungu ni vyenye haki, na kulingana na tabia Yake na mahitaji ya kazi Yake, kwamba Anafanya kazi kulingana na mpango Wake kwa wokovu wa mwanadamu, na kwamba Yeye ndiye Mungu mwenye haki anayempenda mwanadamu, na kumwokoa mwanadamu, na Anayemhukumu na kumwadibu mwanadamu. Kama utajua tu kwamba wewe ni mwenye hadhi ya chini, na kwamba umepotoka na hutii, lakini hujui kwamba Mungu angependa kuweka wazi wokovu Wake kupitia kwa hukumu na kuadibu ambako Anafanya ndani yako leo, basi huna njia yoyote ya kupitia haya, isitoshe huwezi kuendelea mbele. Mungu hajaja kuua, au kuangamiza, lakini kuhukumu, kulaani, kuadibu, na kuokoa. Kabla ya hitimisho ya mpango Wake wa usimamizi wa miaka 6,000—kabla ya Yeye kuweka wazi mwisho wa kila aina ya binadamu—kazi ya Mungu ulimwenguni ni kwa ajili ya wokovu, yote haya ni ili kuwafanya wale wanaompenda Yeye kukamilika kabisa, na kuwarejesha katika utawala Wake. Kwenye macho ya mwanadamu, wokovu ni upendo wa Mungu, na upendo wa Mungu hauwezi kuwa kuadibu, kuhukumu, na kulaani; wokovu lazima uwe na upendo, huruma, na, zaidi ya hayo, maneno ya faraja, na lazima wokovu uwe na baraka zisizo na mipaka kutoka kwa Mungu. Watu husadiki kwamba wakati Mungu anapomwokoa mwanadamu Anafanya hivyo kwa kumgusa yeye na kumfanya yeye kuutoa moyo wake na kumpa Yeye kupitia kwa baraka na neema Zake. Hivyo ni kusema, Anapomgusa mwanadamu Anamwokoa yeye. Wokovu kama huu ni wokovu ambao shughuli ya biashara inafanywa. Pale tu ambapo Mungu atampa yeye mara mia ndipo mwanadamu anaponyenyekea kwa jina la Mungu, na kulenga kuwa na mienendo mizuri mbele ya Mungu na kumletea Yeye utukufu. Haya si mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu. Mungu amekuja kufanya kazi ulimwenguni ili kumwokoa mwanadamu aliyepotoka—hakuna uongo katika haya; kama upo, Asingefanya kazi Yake yeye Mwenyewe. Kitambo, mbinu Zake za wokovu zilikuwa kuonyesha upendo na huruma mkuu, kiasi cha kwamba Alijitolea Yake yote kwa Shetani ili naye aweze kuwapata wanadamu wote. Leo haifanani kamwe na kitambo: Leo, wokovu wako unatokea kwenye wakati wa siku za mwisho, wakati wa uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake; mbinu za wokovu wako si upendo wala huruma, lakini kuadibu na hukumu ili mwanadamu aweze kuokolewa kabisa. Hivyo basi, kila kitu unachopokea ni kuadibu, hukumu, na kupiga bila huruma, lakini jua kwamba katika kupiga huku kusiko na huruma hakuna hata adhabu ndogo zaidi, jua kwamba licha ya namna ambavyo maneno haya yanavyoweza kuwa makali, kile kinachokupata ni maneno machache yanayoonekana kutokuwa na huruma kabisa kwako, na jua kwamba, licha ya namna ambavyo hasira Yangu itakavyokuwa, kile kitakachokujia bado ni maneno ya mafunzo, na sinuii kukudhuru, au kukuua. Je, haya yote ni ukweli, sivyo? Jua kwamba leo, haijalishi kama kutakuwa na kuhukumu kwa haki au utakasaji usio na huruma na kuadibu, yote haya ni kwa minajili ya wokovu. Haijalishi kama leo kunao uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake, au uwekaji wazi wa aina za mwanadamu, matamko yote ya Mungu na kazi ni kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaompenda Mungu kwa dhati. Kuhukumu kwa haki ni kwa ajili ya kumtakasa mwanadamu, utakasaji usio na huruma ni kwa ajili ya kumsafisha mwanadamu, maneno makali au kuadibu yote ni kwa ajili ya kutakasa, na kwa minajili ya wokovu. Na hivyo, mbinu ya leo ya wokovu haifanani na ya kitambo. Leo, kuhukumu kwa haki kunakuokoa wewe, na ni zana nzuri pia ya kumuainisha kila mmoja wenu kulingana na aina, na kuadibu kusiko na huruma kunawaletea wokovu mkubwa—na ni kipi ambacho unahitajika kusema mbele ya kuadibu na kuhukumu huku? Je, hujafurahia wokovu kutoka mwanzo hadi mwisho? Nyote mmeona Mungu mwenye mwili na kutambua kudura na hekima Yake; zaidi ya hayo, umepitia hali ya kupigwa na kufundishwa nidhamu mara kwa mara. Lakini je, hujapokea pia neema kubwa? Je, baraka zako si kubwa zaidi kuliko za mtu yeyote mwengine? Neema zako ni nyingi zaidi kuliko utukufu na utajiri ulioofurahiwa na Sulemani! Hebu fikiria: Kama nia Yangu ya kuja ulimwenguni ingekuwa ni kushutumu na kukuadhibu wewe, na wala si kukuokoa, je, siku zako zingedumu kwa muda mrefu? Mngeweza, enyi viumbe wenye dhambi wa mwili na damu, kuishi hadi leo? Kama ingekuwa tu ni kwa ajili ya kuwaadhibu nyinyi, kwa nini Nikawa mwili na kuanza kushughulikia shughuli kubwa kama hiyo? Je, lisingekuwa neno moja tu ambalo Ningetumia kuwaadhibu nyinyi viumbe wenye kufa tu? Ningekuwa bado na akili ya kukuangamiza baada ya kukushutumu? Je, bado husadiki maneno haya Yangu? Ningeweza kumwokoa mwanadamu kupitia tu kwa upendo na huruma? Au Ningetumia tu kusulubishwa kwa minajili ya kumwokoa mwanadamu? Je, tabia Yangu yenye haki si nzuri zaidi ya kumfanya mwanadamu kuwa mtiifu kabisa? Je, haiwezi kabisa kumwokoa mwanadamu zaidi?
Ingawa maneno Yangu yanaweza kuwa makali, yote yanasemwa kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, kwa kuwa Ninazungumza tu maneno na sio kuuadhibu mwili wa mwanadamu. Maneno haya humsababisha mwanadamu kuishi katika nuru, kujua kwamba mwanga upo, kujua kwamba mwanga ni wa thamani, hata zaidi kujua jinsi maneno haya yalivyo na manufaa kwa mtu, na kujua kwamba Mungu ni wokovu. Ingawa Nimesema maneno mengi ya kuadibu na hukumu, hayajafanywa kwako katika vitendo. Nimekuja kufanya kazi Yangu, kuzungumza maneno Yangu na, ingawa maneno Yangu yanaweza kuwa magumu, yanasemwa kwa hukumu ya upotovu na uasi wako. Madhumuni Yangu ya kufanya hili yanabaki kumwokoa mtu kutoka kwa utawala wa Shetani, kutumia maneno Yangu ili kumwokoa mwanadamu; Kusudi Langu sio kumdhuru mwanadamu kwa maneno Yangu. Maneno Yangu ni makali ili matokeo yaweze kupatikana kutoka katika Kazi Yangu. Ni katika kufanya kazi kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kujijua na anaweza kujitenga mbali na tabia yake ya uasi. Umuhimu mkubwa zaidi wa kazi ya maneno ni kuwaruhusu watu kuweza kutia katika matendo ukweli baada ya kuuelewa ukweli, kutimiza mabadiliko katika tabia yao, na kutimiza maarifa kuhusu wao wenyewe na kazi ya Mungu. Mbinu za kufanya kazi tu kupitia kwa kuongea ndizo zinazoweza kuleta mawasiliano kuhusu uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu, maneno tu ndiyo yanayoweza kuelezea ukweli. Kufanya kazi kwa njia hii ndiyo mbinu bora zaidi ya kumshinda mwanadamu; mbali na matamko ya maneno, hakuna mbinu nyingine inayoweza kumpatia mwanadamu uelewa wa wazi zaidi wa ukweli na kazi ya Mungu, na hivyo basi katika awamu Yake ya mwisho ya kazi, Mungu anazungumza naye mwanadamu ili kuweza kuwa wazi kwa mwanadamu kuhusu ukweli na siri zote ambazo haelewi, na hivyo basi kumruhusu kufaidi njia ya kweli na uzima kutoka kwa Mungu na kisha kutosheleza mapenzi ya Mungu. Madhumuni ya kazi ya Mungu juu ya mwanadamu ni ili aweze kukidhi mapenzi ya Mungu na yote yamefanywa kumwokoa mwanadamu, kwa hivyo wakati wa wokovu wake wa mwanadamu Yeye hafanyi kazi ya kumwadibu mtu. Wakati wa wokovu wa mwanadamu, Mungu haadhibu maovu au kulipa mema, wala Yeye hafunui hatima ya aina zote za watu. Badala yake, ni baada tu ya hatua ya mwisho ya kazi Yake kukamilishwa ndipo basi Atafanya kazi ya kuadhibu maovu na kulipa mazuri, na kisha basi ndipo Atafunua mwisho wa aina zote za watu. Wale ambao wanaadhibiwa hakika hawataweza kuokolewa, wakati wale waliookolewa watakuwa wale ambao wamepata wokovu wa Mungu wakati wa wokovu Wake wa mwanadamu. Wakati wa kazi ya Mungu ya wokovu, wale wote ambao wanaweza kuokolewa wataokolewa kwa upeo wa juu zaidi, hakuna hata mmoja wao atakayeachwa, kwa kuwa kusudi la kazi ya Mungu ni kumwokoa mwanadamu. Wote ambao, wakati wa wokovu wa Mungu wa mwanadamu, hawawezi kufikia mabadiliko katika tabia zao, wote ambao hawawezi kumtii Mungu kabisa, wote watakuwa walengwa wa adhabu. Hatua hii ya kazi—kazi ya maneno—humwekea wazi mwanadamu njia na siri zote ambazo haelewi, ili mwanadamu aweze kuelewa mapenzi ya Mungu na mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu, ili aweze kuwa katika ile hali ya kutia katika matendo maneno ya Mungu na kutimiza mabadiliko hayo katika tabia yake. Mungu huyatumia maneno tu kufanya kazi Yake, na hawaadhibu watu kwa sababu ni waasi kidogo, kwa sababu sasa ndio wakati wa kazi ya wokovu. Kama kila mtu ambaye alikuwa muasi angeadhibiwa, basi hakuna mtu ambaye angepata fursa ya kuokolewa; wote wangeadhibiwa na kuanguka kuzimuni. Kusudi la maneno ya yanayomhukumu mtu ni kumwezesha kujitambua na kumtii Mungu; sio kwao kuadhibiwa kwa njia ya hukumu ya maneno. Wakati wa kazi ya maneno, watu wengi watafunua uasi wao na kutotii kwao, na wataweka wazi kutotii kwao kwa Mungu mwenye mwili. Lakini Yeye hatawaadhibu watu hawa wote kwa sababu ya hili, badala yake Atawatupa kando wale ambao wamepotoka kabisa na ambao hawawezi kuokolewa. Atautoa mwili wao kwa Shetani, na katika hali kadhaa, kumaliza mwili wao. Wale ambao wanaachwa wataendelea kufuata na kupitia kushughulikiwa na kupogolewa. Ikiwa wanapofuata hawawezi kukubali kushughulikiwa na kupogolewa na wanazidi kupotoka, basi watu hawa watapoteza nafasi zao za wokovu. Kila mtu ambaye amekubali ushindi wa maneno atakuwa na nafasi nzuri ya wokovu. Wokovu wa Mungu wa kila mmoja wa watu hawa huwaonyesha upole Wake mkubwa, kumaanisha kwamba wanaonyeshwa uvumilivu mkubwa. Mradi watu warudi kutokakatika njia mbaya, mradi kama waweze kutubu, basi Mungu atawapa fursa ya kupata wokovu wake. Watu wanapoasi dhidi ya Mungu kwanza, Mungu hana hamu ya kuwaua, lakini badala yake Anafanya yote Anayoweza kuwaokoa. Ikiwa mtu kwa kweli hana nafasi ya wokovu, basi Mungu atamtupa pembeni. Kwamba Mungu si mwepesi wa kumwadhibu mtu ni kwa sababu Anataka kuwaokoa wale wote ambao wanaweza kuokolewa. Yeye huwahukumu, huwapa nuru na kuwaongoza watu tu kwa maneno, na Hatumii fimbo kuwaua. Kutumia maneno kuwaokoa watu ni kusudi na umuhimu wa hatua ya mwisho ya kazi.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni