1/29/2018

Wale Ambao Tabia Yao Imebadilika Ndio Wanaoingia Katika Uhalisi wa Ukweli

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu

Neno-Laonekana-katika-Mwili

Wale Ambao Tabia Yao Imebadilika Ndio Wanaoingia Katika Uhalisi wa Ukweli


Mwenyezi Mungu alisema, Njia ambayo Roho Mtakatifu huchukua ndani ya watu ni kuvuta kwanza mioyo yao kutoka kwa watu, matukio, na vitu vyote, na kuingiza ndani ya maneno ya Mungu ili ndani ya mioyo yao wote waamini kwamba maneno ya Mungu hayana shaka kabisa na ni kweli kabisa. Kwa vile unaamini katika Mungu lazima uamini katika maneno Yake; ikiwa umeamini katika Mungu kwa miaka mingi lakini hujui njia ambayo Roho Mtakatifu hufuata, wewe kweli ni muumini? Ili kutimiza maisha ya mtu wa kawaida na maisha yanayofaa ya mtu na Mungu, lazima kwanza uamini maneno Yake.
Ikiwa hujakamilisha hatua ya kwanza ya kazi ambayo Roho Mtakatifu hufanya ndani ya watu, huna msingi. Unakosa kanuni ya msingi kabisa, kwa hiyo unawezaje kutembea njia iliyo mbele? Kufuata njia sahihi ya Mungu kumkamilisha mwanadamu ni kuingia katika njia sahihi ya kazi halisi ya Roho Mtakatifu; pia ni kufuata njia ambayo Roho Mtakatifu hutembea. Hivi sasa, njia ambayo Roho Mtakatifu hutembea ni maneno halisi ya Mungu. Kwa hiyo, kwa mtu kuitembea, ni lazima atii, na kula na kunywa maneno halisi ya Mungu mwenye mwili. Anafanya kazi ya maneno, na kila kitu kinanenwa kutoka kwa maneno Yake, na kila kitu kinaanzishwa juu ya maneno Yake, maneno Yake halisi. Kama ni kuwa bila shaka yoyote kabisa kuhusu Mungu kuwa mwili au kumjua Yeye, mtu anapaswa kuweka bidii zaidi katika maneno Yake. Vinginevyo, hawezi kutimiza chochote kamwe, na ataachwa bila chochote. Ni kwa kuja kumjua Mungu tu na kumridhisha kwa msingi wa kula na kunywa maneno Yake ndipo mtu anaweza kuanzisha polepole uhusiano unaofaa na Yeye. Kula na kunywa maneno Yake na kuyaweka katika matendo ni ushirikiano bora zaidi na Mungu, na ni kitendo kinachotoa ushuhuda vizuri zaidi kama mmoja wa watu Wake. Mtu akielewa na aweze kutii kiini cha maneno halisi ya Mungu, anaishi katika njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu na ameingia katika njia sahihi ya Mungu kumkamilisha mwanadamu. Zamani ilikuwa kwamba watu walitafuta neema na walitafuta amani na furaha, na kisha waliweza kupata kazi ya Mungu. Ni tofauti sasa. Ikiwa hawana maneno ya Mungu aliyepata mwili, ikiwa hawana uhalisi wa maneno hayo, hawawezi kupata kibali kutoka kwa Mungu na wataondoshwa na Mungu. Ili kutimiza maisha ya kiroho ya kufaa, kwanza kula na kunywa maneno ya Mungu na kuyaweka katika vitendo; na juu ya msingi huu anzisha uhusiano wa kufaa kati ya mwanadamu na Mungu. Ni vipi ambavyo unashirikiana? Ni vipi ambavyo unakuwa shahidi kama mmoja wa watu Wake? Ni vipi ambavyo unaanzisha uhusiano wa kufaa na Mungu?

Hivi ndivyo namna ya kuona ikiwa una uhusiano wa kufaa na Mungu katika maisha yako ya kila siku:

1. Unaamini ushuhuda wa Mungu mwenyewe?
2. Unaamini katika moyo wako kwamba maneno ya Mungu ni kweli na yasiyoweza kukosea?
3. Wewe ni mtu unayeweka maneno Yake katika vitendo?
4. Umejitolea kwa kile Alichokuaminia? Unawezaje kujitolea kwa hicho?
5. Je, kila kitu unachofanya ni kwa ajili ya kumridhisha na kuwa mwaminifu kwa Mungu?
Kupitia mambo haya, unaweza kutathmini ikiwa una uhusiano wa kufaa na Mungu katika hatua hii ya sasa.
Ikiwa unaweza kukubali kile Mungu anakuaminia wewe, kukubali ahadi Yake, na kufuata njia ya Roho Mtakatifu, hii ni kutekeleza mapenzi ya Mungu. Una uwazi wa ndani kuhusu njia ya Roho Mtakatifu? Je, matendo yako ya sasa ni ya kufuatana na njia Yake? Moyo wako unasonga karibu na Mungu? Uko radhi kuifuata nuru mpya kabisa kutoka kwa Roho Mtakatifu? Uko radhi kupatwa na Mungu? Uko radhi kuwa dhihirisho la utukufu wa Mungu duniani? Una nia ya kutimiza anachohitaji Mungu? Ikiwa una hiari ya kushirikiana mara tu Mungu anapozungumza na una hiari ya kumridhisha Yeye, ikiwa huu ni uwezo wako wa ndani, inamaanisha kwamba maneno ya Mungu yamezaa matunda ndani ya moyo wako. Ikiwa huna aina hiyo ya hiari na huna lengo katika kazi yako, inamaanisha kwamba moyo wako bado haujasisimuliwa na Mungu.
Kwa vile watu wameingia rasmi katika mafundisho ya ufalme, masharti ya Mungu kwao yameinuliwa. Mtu anawezaje kuona hilo? Ilisemekana awali kwamba watu hawana uzima, lakini sasa watu wanatafuta uzima, wanatafuta kuwa mmoja wa watu wa Mungu, na kupatwa na kukamilishwa na Mungu. Je, huku sio kuinuliwa? Kwa kweli, masharti kwa watu ni rahisi kuliko yalivyokuwa. Watu hawahitajiki kuwa watendaji huduma au kufa—wanayotakiwa tu ni kuwa watu wa Mungu. Je, hilo si rahisi zaidi? Bora tu uutoe moyo wako kwa Mungu na kutii uongozi Wake, yote yatafaulu. Mbona unadhani ni vigumu sana? Kile kinachozungumziwa sasa kuhusu kuingia katika uzima ni dhahiri zaidi kuliko hapo awali; watu hawakuwa na udhahiri na hawakujua uhalisi wa uzima unahusu nini. Wale walio na athari kwa kusikia maneno ya Mungu, walio na nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, na ambao wamepata kukamilishwa Kwake na mabadiliko katika tabia mbele Yake—watu hawa wote wana uzima. Kila ambacho Mungu anataka ni viumbe wenye uhai, sio vitu visivyo na uhai. Ikiwa huna uhai, huna uzima, na Mungu hatanena nawe, na hasa Hatakuinua kuwa mmoja wa watu Wake. Kwa vile mmeinuliwa na Mungu, kwa vile mmepokea baraka kubwa kama hii kutoka Kwake, hii inamaanisha kwamba nyinyi nyote ni watu walio na uzima, na wale walio na uzima hutoka kwa Mungu.
Ili mtu kufuatilia mabadiliko katika tabia ya maisha yake, njia ya kutenda ni rahisi. Ikiwa unaweza kufuata maneno halisi ya Roho Mtakatifu katika uzoefu wako wa utendaji, utaweza kutimiza mabadiliko katika tabia yako. Ikiwa utafuata na kutafuta chochote ambacho Roho Mtakatifu husema, wewe ni mtu anayemtii Yeye, na kwa njia hii utaweza kuwa na mabadiliko katika tabia. Tabia ya mwanadamu hubadilika na maneno halisi ya Roho Mtakatifu; ikiwa kila mara wewe hutetea uzoefu wako wa zamani na sheria, tabia yako haitabadilika. Ikiwa Roho Mtakatifu angezungumza leo kuwaambia watu wote waingie katika uzima wa ubinadamu wa kawaida lakini ukaendelea kulenga sehemu ya juu na kuchanganyikiwa kuhusu uhalisi na usiuchukulie kwa makini, utakuwa mtu ambaye haendelei na kazi Yake na hutakuwa mtu aliyeingia katika njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu. Ikiwa tabia yako inaweza kubadilika au la inategemea na ikiwa unaweza kuendelea na maneno halisi ya Roho Mtakatifu au la na una ufahamu wa kweli. Hili ni tofauti na kile mlichoelewa awali. Kile ulichoelewa kuhusu mabadiliko katika tabia awali kilikuwa kwamba wewe, ambaye ni rahisi kuhukumu, kupitia kwa kufundishwa nidhamu na Mungu huzungumzi ovyo ovyo tena. Lakini hii ni hali moja tu ya mabadiliko, na hivi sasa suala muhimu zaidi ni kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu. Unafuata chochote asemacho Mungu; unatii chochote asemacho Yeye. Watu hawawezi kubadilisha tabia yao wenyewe; lazima wapitie hukumu na kuadibu na usafishaji wa uchungu wa maneno ya Mungu, au kushughulikiwa, kufunzwa nidhamu, na kupogolewa na maneno Yake. Ni baada ya hapo tu ndipo wanaweza kutimiza utiifu na ibada kwa Mungu, na sio kujaribu kumdanganya Yeye na kumshughulikia kwa uzembe. Ni kupitia kwa usafishaji wa maneno ya Mungu ndio watu hupata mabadiliko katika tabia. Ni wale tu wanaopitia mfichuo, hukumu, kufundishwa nidhamu, na kushughulikiwa kwa maneno Yake ambao hawatathubutu tena kufanya mambo kwa kutojali, na watakuwa watulivu na makini. Jambo muhimu sana ni kwamba wanaweza kutii maneno halisi ya Mungu na kutii kazi ya Mungu, na hata kama hayalingani na fikira za binadamu, wanaweza kuyaweka kando na kutii kwa makusudi. Mabadiliko katika tabia yalipozungumziwa hapo awali, imekuwa hasa kuhusu kujinyima mwenyewe, kuruhusu mwili kuteseka, kufunza nidhamu mwili wa mtu, na kujiondolea mapendeleo ya mwili—hii ni aina moja ya mabadiliko katika tabia. Watu sasa wanajua kwamba maonyesho halisi ya mabadiliko katika tabia ni kutii maneno halisi ya Mungu na vilevile kuweza kuwa na ufahamu halisi wa kazi Yake mpya. Kwa njia hii watu wataweza kuondoa ufahamu wao wa awali wa Mungu katika fikira zao, na kutimiza ufahamu wa kweli wa na utiifu Kwake. Hii tu ndio maonyesho halisi ya mabadiliko katika tabia.
Kufuatilia kwa watu kuingia katika uzima kunalingana na maneno ya Mungu; imesemwa hapo awali kwamba kila kitu hutimizwa kwa sababu ya maneno Yake, lakini hakuna aliyeona ukweli. Ikiwa katika hatua hii utaingia katika uzoefu utakuwa wazi kabisa—huku ni kujenga msingi mzuri kwa majaribio ya siku za baadaye, na haijalishi anachosema Mungu, unatakiwa tu kuingia katika maneno Yake. Mungu anaposema Anaanza kuadibu watu, unakubali kuadibu Kwake. Mungu anapowauliza watu wafe, unakubali jaribio hilo. Ikiwa kila mara unaishi ndani ya matamshi Yake mapya zaidi, mwishowe maneno ya Mungu yatakukamilisha wewe. Kadri unavyoingia katika maneno ya Mungu, ndivyo utakavyokamilisha haraka zaidi. Kwa nini Ninawasiliana tena na tena na kuwaambia muelewe na kuingia katika maneno ya Mungu? Ni kwa kulenga tu kazi yako kwa maneno ya Mungu na kuyapitia na kuingia katika uhalisi wake ndipo Roho Mtakatifu atakuwa na nafasi ya kufanya kazi ndani yako. Kwa hiyo nyote ni washindani katika kila mbinu ya kazi ya Mungu, na haijalishi ikiwa mateso yenu yamekuwa makubwa au madogo mwishowe, nyote mtapata hidaya. Ili kutimiza ukamilifu wenu wa mwisho, lazima muingie katika maneno yote ya Mungu. Kwa Roho Mtakatifu kuwakamilisha watu, Hafanyi kazi kwa upande mmoja tu. Anahitaji ushirikiano wa watu; Anahitaji kila mtu ashirikiane Naye kwa makusudi. Haijalishi anachosema Mungu, unaingia tu katika maneno Yake—hii ni ya manufaa zaidi kwa maisha yenu. Kila kitu ni kwa ajili ya mabadiliko yenu katika tabia. Unapoingia katika maneno ya Mungu, moyo wako utasisimuliwa na Mungu, na utaweza kuelewa kila kitu ambacho Mungu anataka kutimiza katika hatua hii ya kazi, na utakuwa na nia ya kukitimiza. Katika nyakati za kuadibu, baadhi ya watu waliamini kwamba hiyo ilikuwa mbinu ya kazi na hawakuamini katika maneno ya Mungu. Kutokana na hilo, hawakupitia usafishaji na wakatoka katika nyakati za kuadibu bila kupata chochote na hawakuelewa chochote. Kuna baadhi ambao huingia kwa hakika katika maneno haya bila chembe ya shaka yoyote; wanasema kuwa maneno ya Mungu ni kweli na yasioweza kukosea na kwamba watu wanapaswa kuadibiwa. Wanang’ang’ana katika hili kwa kipindi fulani cha wakati na kuachilia siku zao za baadaye na majaliwa yao, na wanapotoka tu hapo tabia yao huwa imebadilika vilivyo na wao huwa na hata ufahamu wa kina zaidi kuhusu Mungu. Wale ambao wametoka katikati ya kuadibu wote huhisi kupendeza kwa Mungu, na wanajua kwamba hatua hiyo ya kazi ya Mungu ni upendo Wake mkuu ukija juu ya wanadamu, kwamba ni ushindi na wokovu wa upendo wa Mungu. Nao pia husema kwamba mawazo ya Mungu ni mazuri kila mara, na kila jambo ambalo Mungu hufanya ndani ya mwanadamu ni upendo, sio chuki. Wale wasioamini maneno ya Mungu au kuyachukulia kuwa muhimu hawakupitia usafishaji katika nyakati za kuadibu, na matokeo yake ni kwamba Roho Mtakatifu haandamani nao, na hawajapata chochote. Kwa wale walioingia katika nyakati za kuadibu, ingawa walipitia usafishaji, Roho Mtakatifu alikuwa anafanya kazi ndani yao kwa njia iliyofichika, na matokeo ni kwamba walipitia mabadiliko katika tabia yao ya maisha. Watu wengine huonekana kuwa wazuri sana kwa nje. Kila mara wao huwa na furaha, lakini hawajaingia katika hali hiyo ya usafishaji wa maneno ya Mungu na hawajabadilika kamwe, ambayo ni matokeo ya kutoamini maneno ya Mungu. Ikiwa huamini maneno Yake Roho Mtakatifu hatafanya kazi ndani yako. Mungu huonekana kwa wote wanaoamini maneno Yake; wale wanaoamini na kufahamu maneno Yake watapata upendo Wake!
Ingia katika hali ya maneno ya Mungu, lenga kuifanya kwa njia ya kutenda, na utafute kinachopaswa kuwekwa katika matendo; ni kwa kufanya hivyo tu ndipo utakuwa na mabadiliko katika tabia ya maisha yako. Ni kwa njia hii tu ndiyo utaweza kukamilishwa na Mungu, na ni watu tu ambao wamekamilishwa na Mungu kwa njia hiyo ambao wanaweza kuwa sambamba na mapenzi Yake. Kupokea nuru mpya, lazima uishi ndani ya maneno Yake. Ikiwa umesisimuliwa na Roho Mtakatifu mara moja pekee, hiyo haitoshi kamwe—lazima uzame ndani zaidi. Wale ambao wamesisimuliwa mara moja pekee ari iliyo ndani yao imeamshwa hivi karibuni na wanakuwa radhi kutafuta, lakini hawawezi kudumisha hilo kwa kipindi kirefu, na lazima wapokee kila mara kusisimuliwa na Roho Mtakatifu. Kuna nyakati nyingi Nimetaja kuwa Natarajia kwamba Roho wa Mungu aweze kusisimua roho za watu, kwamba wafuatilie mabadiliko katika tabia ya maisha yao, na wanapotafuta kusisimuliwa na Mungu wafahamu udhaifu wao, na kwamba wakati wa kupitia maneno Yake, waondoe mambo machafu ndani yao (kujidai, kiburi, na fikira zao wenyewe, na kadhalika.) Usiamini kwamba kupokea tu kwa utendaji nuru mpya kunafaa—lazima pia uachane na vitu kutoka kwa hali mbaya. Hamhitaji tu kuingia kutoka kwa hali nzuri, lakini pia mnahitaji kujisafisha wenyewe kutoka kwa mambo yote machafu katika hali mbaya. Lazima ujichunguze siku zote na uone ni mambo yapi machafu bado yako ndani yako. Fikira za watu za kidini, makusudi, matarajio, kujidai, na kiburi yote ni mambo machafu. Jilinganishe na maneno yote ya Mungu ya ufunuo, na ujiangalie ndani yako kuona fikira zozote za kidini unazoshikilia, Ukizitambua tu ndipo unaweza kuziacha. Baadhi ya watu husema kwamba sasa inatosha tu kufuata nuru ya kazi ya wakati huu ya Roho Mtakatifu na hakuna kitu kingine kinachotakiwa kusikizwa. Basi ni vipi ambavyo utaondoa fikira zako za kidini zinapojitokeza? Unadhani ni rahisi hivyo kufuata maneno ya Mungu? Ndani ya maisha yako halisi, bado kuna mambo ya kidini yanayoweza kuwa ya kuvuruga, na mambo haya yanapojitokeza, yanaweza kuvuruga uwezo wako wa kukubali mambo mapya. Haya yote ni matatizo ambayo huwepo kwa kweli. Ikiwa utafuatilia tu maneno halisi ya Roho Mtakatifu huwezi kuridhisha mapenzi ya Mungu. Unapofuatilia nuru ya sasa ya Roho Mtakatifu, unapaswa kutambua ni fikira na makusudi gani ambayo bado unashikilia, ni kujidai gani kwa binadamu kupo hasa, na ni mienendo gani inakosa kumtii Mungu. Na baada ya kutambua mambo haya yote, lazima uachane nayo. Kukufanya wewe utupe matendo na mienendo yako ya awali yote ni kwa ajili ya kuyafuata maneno ya sasa ya Roho Mtakatifu. Kwa mabadiliko katika tabia, kwa upande mmoja, yanatimizwa kupitia kwa maneno ya Mungu, na kwa upande mwingine, yanahitaji watu washirikiane. Yaani, kazi ya Mungu na kutenda kwa watu vyote ni vya lazima.
Katika njia yako ya baadaye ya huduma, unawezaje kuridhisha mapenzi ya Mungu?
Jambo moja muhimu ni kufuatilia kuingia katika uzima, kufuatilia mabadiliko katika tabia, na kufuatilia kuingia kwa kina zaidi ndani ya ukweli—hii ndiyo njia ya kutimiza kufanywa mkamilifu na kupatwa na Mungu. Nyote mnapaswa kupokea agizo la Mungu, kwa hiyo ni nini hicho? Hii inahusiana na hatua inayofuata ya kazi, ambayo itakuwa kazi kuu zaidi itakayotekelezwa kotekote katika ulimwengu mzima. Kwa hiyo sasa mnapaswa kufuatilia mabadiliko katika tabia yenu ya maisha ili muwe kweli thibitisho la Mungu kupata utukufu kupitia kwa kazi Yake katika siku za baadaye, na kufanywa kuwa vielelezo vya kazi Yake ya siku za baadaye. Kazi yote ya leo inaweka msingi kwa ajili ya kazi ya siku za baadaye; ni kwa wewe kutumiwa na Mungu na ili uweze kuwa na ushuhuda Wake. Ikiwa hii ni chombo cha kazi yako, utaweza kupata uwepo wa Roho Mtakatifu. Kadri chombo cha kazi yako kilivyo juu, ndivyo itawezekana kwako wewe kukamilishwa zaidi. Kadri unavyofuatilia ukweli, ndivyo Roho Mtakatifu atafanya kazi zaidi. Kadri unavyokuwa na nguvu zaidi kwa kazi, ndivyo utakavyopata zaidi. Roho Mtakatifu huwakamilisha watu kulingana na hali yao ya ndani. Baadhi ya watu husema kwamba hawako radhi kutumiwa na Mungu au kukamilishwa na Yeye, kwamba itakuwa sawa ikiwa watakuwa na amani ndani ya mwili, na wasipatwe na misiba mikuu yoyote. Watu wengine hawako radhi kuingia katika ufalme, lakini wako radhi kushuka katika shimo la kuzimu, na Mungu atakutimizia hilo pia. Chochote unachofuatilia ndicho Mungu atatimiza. Kwa hiyo unafuatilia nini sasa? Je, unafuatilia kukamilishwa? Matendo na mienendo yako ya sasa ni kwa ajili ya kufanywa mkamilifu na Mungu, kwa ajili ya kupatwa na Yeye? Ni lazima siku zote ujipime kwa njia hii katika maisha yako ya kila siku. Ukilenga moyo wako katika kufuatilia lengo moja, Mungu bila shaka atakukamilisha. Hii ni njia ya Roho Mtakatifu. Njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu inapatikana kupitia kwa kutafuta kwa watu. Kadri unavyotamani kukamilishwa na kupatwa na Mungu, ndivyo Roho Mtakatifu atafanya kazi zaidi ndani yako. Kadri usivyotafuta, na kadri unavyokuwa mbaya na kukimbia, ndivyo zaidi Roho Mtakatifu anakosa nafasi za kufanya kazi. Roho Mtakatifu atakuacha polepole. Uko radhi kukamilishwa na Mungu? Uko radhi kupatwa na Mungu? Uko radhi kutumiwa na Mungu? Mnapaswa kufuatilia kufanya kila kitu kwa ajili ya kukamilishwa, kupatwa, na kutumiwa na Mungu, kuruhusu kila kitu katika ulimwengu kuona matendo ya Mungu yakifichuliwa ndani yenu. Miongoni mwa mambo yote, nyinyi ni watawala wa hayo, na miongoni mwa yote yaliyopo, mtamruhusu Mungu kupata ushuhuda Wake na utukufu Wake kwa sababu yenu—hii inaonyesha kwamba nyinyi ni kizazi kilichobarikiwa zaidi.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni