9/04/2017

Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu


Enzi ya zama ishaenda, na enzi mpya imefika. Mwaka baada ya mwaka na siku baada ya siku, Mungu amefanya kazi nyingi. Alikuja duniani , kisha Akatoka. Mzunguko kama huu umeendelea kwa vizazi vingi. Siku ya leo, Mungu anaendelea kama mbeleni kufanya kazi Anayopaswa kufanya, kazi ambayo bado Hajaikamilisha, kwani hadi leo, bado Hajaingia mapumzikoni. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo, Mungu amefanya kazi nyingi, lakini unajua kwamba kazi anayoifanya Mungu leo ni nyingi kuliko awali na kipimo ni kikubwa zaidi? Hii ndiyo maana Nasema Mungu amefanya jambo kubwa miongoni mwa wanadamu. Kazi zote za Mungu ni muhimu sana, iwe kwa mwanadamu ama Mungu, kwani kila kitu cha kazi Yake kina uhusiano na mwanadamu.
Sababu kazi ya Mungu haiwezi kuonekana wala kuguswa, wala haiwezi kuonwa na ulimwengu, basi jinsi gani ikawa kitu kikubwa? Ni jambo gani linachukuliwa kuwa kubwa? Hakika hakuna anayeweza kukataa kuwa kazi zote za Mungu zinaweza kuchukuliwa kuwa kubwa, lakini mbona Nasema kazi anayofanya Mungu leo iko hivi? Ninaposema Mungu amefanya kitu kikubwa, hii bila shaka inahusisha siri nyingi ambazo mwanadamu bado hajazielewa. Wacha tuyazungumzie sasa.
Yesu alizaliwa horini wakati ambao hungevumilia kuwepo Kwake, lakini dunia bado haingesimama katika njia Yake, na Aliishi miongoni mwa wanadamu kwa miaka thelathini na tatu chini ya ulinzi wa Mungu. Kwa miaka hiyo yote ya maisha, Alikuwa na uzoefu wa uchungu wa dunia na Akaonja maisha ya taabu ya dunia. Alilichukua jukumu zito la kusulubiwa ili kuwakomboa wanadamu wote. Aliwakomboa wote wenye dhambi walioishi chini ya miliki ya Shetani, na mwishowe, mwili Wake uliofufuka ukarudi mahali Pake pa mapumziko. Sasa kazi mpya ya Mungu imeanza, na pia ni mwanzo wa enzi mpya. Mungu analeta nyumbani Kwake wale waliokombolewa kuanza kazi Yake ya wokovu. Wakati huu, kazi ya wokovu ni ya kina kuliko mbeleni. Haitafanywa na Roho Mtakatifu akifanya kazi ndani ya mwanadamu ili kumruhusu kubadilika mwenyewe, wala haitafanywa kupitia mwili wa Yesu Akijitokeza miongoni mwa wanadamu, na haitafanywa hata kidogo kwa namna ingine. Badala yake, kazi itafanywa na kuongozwa na Mungu mwenye mwili Mwenyewe. Hii inafanywa ili kumwongoza binadamu katika kazi mpya. Hili si jambo zuri? Mungu Hafanyi kazi hii kupitia sehemu ya wanadamu ama unabii, lakini kwa Mungu Mwenyewe. Wengine wanaweza kusema kuwa hili si jambo kubwa na haliwezi kumletea mwanadamu furaha. Hata hivyo, Nitakuambia kwamba kazi ya Mungu siyo tu hii, ila kitu kikubwa zaidi na kingi zaidi.
Wakati huu, Mungu haji kufanya kazi kwa mwili wa kiroho ila kwa ile kawaida sana. Sio tu mwili wa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, lakini pia mwili ambao Mungu anarudia. Ni mwili wa kawaida sana. Ndani Yake, huwezi kuona chochote kilicho tofauti na cha wengine, lakini unaweza kupokea kutoka Kwake ukweli ambao hujawahi kusikia mbeleni. Mwili huu usio na umuhimu ni mfano halisi wa maneno yote ya kweli kutoka kwa Mungu, ambao hufanya kazi ya Mungu siku za mwisho, na maonyesho ya tabia nzima ya Mungu kwa mwanadamu kuja kujua. Je, hukutamani sana kumwona Mungu aliye mbinguni? Je, hukutamani sana kumwelewa Mungu aliye mbinguni? Je, hukutamani sana kuona hatima ya mwanadamu? Atakueleza hizi siri zote ambazo hazijaelezwa, na hata Atakuelezea kuhusu ukweli usioelewa. Yeye ndiye lango la kuingia katika ufalme, na kiongozi wako katika enzi mpya. Mwili wa kawaida kama huu una siri nyingi zisizoeleweka. Matendo Yake labda hayaeleweki kwako, lakini lengo la kazi yote Anayoifanya limekutosha kuona kuwa Yeye si mwili wa kawaida anavyoamini mwanadamu. Kwani Anawakilisha mapenzi ya Mungu na pia ulinzi Anaoonyesha Mungu kwa mwanadamu siku za mwisho. Ingawa huwezi kuyasikia maneno Anayozungumza yanayoonekana kutingisha mbingu na dunia wala kuona macho Yake kama moto mkali, na ingawa huwezi kuhisi nidhamu ya fimbo Yake ya chuma, unaweza kusikia kupitia maneno Yake ghadhabu ya Mungu na kujua kwamba Mungu Anaonyesha huruma kwa mwanadamu; unaweza kuona haki ya tabia ya Mungu na hekima Yake, na zaidi ya hayo, kutambua wasiwasi na utunzaji Anao Mungu kwa wanadamu wote, Kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni ya kuruhusu mwanadamu kumwona Mungu Aliye mbinguni akiishi miongoni mwa wanadamu duniani, na kumwezesha mwanadamu kuja kumjua, kumtii, kumheshimu, na kumpenda Mungu. Hii ndiyo maana Amerudi kwa mwili kwa mara ya pili. Ingawa kile anachokiona mwanadamu siku hii ni Mungu aliye sawa na mwanadamu, Mungu aliye na pua na macho mawili, na Mungu asiye wa ajabu, mwishowe, Mungu Atakuonyesha kwamba bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu na dunia zitapitia mabadiliko makuu, bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu zitafifiwa na mwangaza, dunia itakuwa na vurugu, na wanadamu wote wataishi katika kiangazi na tauni. Atakuonyesha kuwa bila wokovu wa Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho, basi Mungu Angekuwa Ashawaangamiza wanadamu wote kuzimu kitambo sana; bila kuwepo kwa mwili huu, basi daima ungekuwa kiongozi wa wenye dhambi na maiti milele. Unapaswa kujua kwamba bila kuwepo kwa mwili huu, wanadamu wote wangetazamia msiba usioepukika na kupata kuwa ngumu kuponyoka adhabu kali zaidi ya Mungu katika siku za mwisho. Bila kuzaliwa kwa mwili huu wa kawaida, nyinyi nyote mngekuwa katika hali ambayo uhai wala kifo havitakuwepo bila kujali jinsi mtakavyovitafuta; bila kuwepo kwa mwili huu, basi siku hii hungeweza kupokea ukweli na kuja mbele ya kiti cha Mungu cha enzi. Badala yake, ungeadhibiwa na Mungu kwa sababu ya dhambi zako zinazotisha. Je, wajua? Kama sio kwa kurudi kwa Mungu kuwa mwili, hakuna ambaye angepata nafasi ya wokovu; na isipokuwa kwa kuja kwa mwili huu, Mungu angekuwa ameimaliza kitambo enzi ya zamani. Hivyo basi, unaweza bado kuukataa kupata mwili kwa mara ya pili kwa Mungu? Sababu unaweza kufaidika sana na huyu mwanadamu wa kawaida, basi mbona hungemkubali kwa urahisi?
Kazi ya Mungu ni ile usiyoweza kuelewa. Kama huwezi kufahamu kama uamuzi wako ni sahihi wala kujua kama kazi ya Mungu inaweza kufaulu, basi mbona usijaribu bahati yako na kuona iwapo huyu mwanadamu wa kawaida ni wa msaada mkubwa kwako, na iwapo Mungu amefanya kazi kubwa. Hata hivyo, lazima Nikuelezee kuwa wakati wa Nuhu, wanadamu walikuwa wamekula na kunywa, wakifunga ndoa na kupeana katika ndoa hadi wakati Mungu asingevumilia kushuhudia, hivyo, Alituma chini mafuriko makubwa kuangamiza wanadamu na kuacha tu nyuma familia ya Nuhu ya watu wanane na aina yote ya ndege na wanyama. Katika siku za mwisho, hata hivyo, wale waliohifadhiwa na Mungu ni wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake hadi mwisho. Ingawa nyakati zote mbili zilikuwa za upotovu mkubwa Asizoweza kuvumilia kushuhudia Mungu, na mwanadamu katika enzi zote mbili alikuwa mpotovu kiasi cha kumkanusha Mungu kama Bwana, watu wote katika wakati wa Nuhu waliangamizwa na Mungu. Mwanadamu katika enzi zote mbili amemhuzunisha Mungu sana, lakini bado Amebakia mvumilivu na wanadamu katika siku za mwisho hadi sasa. Mbona hivi? Hujawahi fikiria haya? Kama kweli hujui, basi wacha Nikuelezee. Sababu Mungu Anaweza kushughulika na wanadamu kwa neema siku za mwisho si kwamba ni wapotovu kidogo zaidi kuliko wanadamu wakati wa Nuhu ama kwamba wamemwonyesha Mungu toba, wala hata si kwamba Mungu Hawezi kuvumilia kuwaangamiza wanadamu katika siku za mwisho ambapo teknolojia imeendelea. Badala yake, ni kwamba Mungu ana kazi ya kufanya kwa kundi la wanadamu katika siku za mwisho na hii itafanywa na Mungu mwenye mwili Mwenyewe. Zaidi ya hayo, Mungu Atachagua sehemu ya kundi hili kama vyombo Vyake vya wokovu, tunda la mpango Wake wa usimamizi, na kuleta wanadamu kama hawa naye katika enzi ifuatayo. Kwa hivyo, bila kujali, hii gharamailiyolipwa na Mungu yote imekuwa katika maandalizi ya kazi Yake ya kupata mwili katika siku za mwisho. Yote uliyonayo siku hii ni kwa sababu ya huu mwili. Ni kwa sababu Mungu Huishi ndani ya mwili ndiyo una nafasi ya kuishi. Hii bahati yote nzuri imepatwa kwa sababu ya huyu mwanadamu wa kawaida. Siyo haya tu, lakini mwishowe kila taifa litamwabudu huyu mwanadamu wa kawaida, na pia kumpa shukrani na kumtii huyu mwanadamu asiye muhimu. Kwa sababu ni Yeye Aliyeleta ukweli, uhai, na njia ya kuwaokoa wanadamu wote, kutuliza migogoro kati ya Mungu na mwanadamu, kuleta Mungu na mwanadamu pamoja karibu na kuwasilisha mawazo kati ya Mungu na mwanadamu. Pia ni Yeye Aliyeleta hata utukufu zaidi kwa Mungu. Mwanadamu wa kawaida kama huyu hastahili uaminifu na ibada yako? Mwili wa kawaida kama huu haufai kuitwa Kristo? Mwanadamu wa kawaida kama huyu Hawezi kuwa maonyesho ya Mungu miongoni mwa wanadamu? Mwanadamu kama huyu Anayesaidia wanadamu kuepuka maafa hastahili mapenzi yako na wewe kumshikilia? Ukiukataa ukweli unaotamkwa na mdomo Wake na pia kuchukia kuwepo Kwake miongoni mwenu, basi nini itakuwa majaliwa yenu?
Kazi yote ya Mungu katika siku za mwisho inafanywa kupitia huyu mwanadamu wa kawaida. Atawapa kila kitu, na juu ya hayo, Anaweza kuamua kila kitu kuwahusu. Mtu kama huyu anaweza kuwa maminivyo: mtu wa kawaida sana asiyestahili kutajwa? Ukweli Wake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ushuhuda wa vitendo vyake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ama ni kuwa njia Anayowaongoza haina thamani ili mfuate? Ni nini kinachowasababisha kumchukia na kumtupilia mbali na kumwepuka? Ni Yeye Anayeonyesha ukweli, ni Yeye Anayetoa ukweli, na ni Yeye Anayewawezesha kuwa na njia ya kusafiri. Inaweza kuwa bado hamwezi pata chembe cha kazi ya Mungu ndani ya ukweli huu? Bila kazi ya Yesu, mwanadamu hangeweza kushuka chini kutoka msalabani, lakini bila kupata mwili siku hii, wale wanaoshuka chini kutoka msalabani hawangewahi kuweza kusifu na Mungu ama kuingia katika enzi mpya. Bila kuja kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi hamngeweza kuwa na hii fursa ama kustahiki kuona uso wa ukweli wa Mungu, kwani nyinyi nyote mngepaswa kuangamizwa kitambo sana. Kwa sababu ya kuja kwa Mungu mwenye mwili mara ya pili, Mungu amewasamehe na kuwaonyesha huruma. Bila kujali, maneno ambayo lazima niwaachie mwishowe ni haya: Huyu mwanadamu wa kawaida, ambaye ni Mungu mwenye mwili, ni wa umuhimu sana kwenu. Hili ni jambo kubwa ambalo Mungu tayari Amefanya miongoni mwa wanadamu.
 Mapendekezo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni