Kanisa la Mwenyezi Mungu |
Matawi yote ya magharibi yanapaswa kuisikiliza sauti Yangu:
Je, mmekuwa waaminifu Kwangu hapo awali? Je, mmekuwa mkiyasikia maneno Yangu mazuri ya ushauri? Je, mnayo matumaini ambayo ni halisi na yasiyo na mashaka? Utiifu wa mwanadamu, mapenzi yake, imani yake—hamna kipatikanacho ila kutoka Kwangu, hamna hata kimoja ila kilichotawazawa na Mimi.
Nyie watu Wangu, myasikiapo maneno Yangu, je mnaielewa nia Yangu? Mnaiona roho Yangu? Mlipoipitia njia ya huduma hapo awali mlikumbana na panda-shuka, maendeleo mazuri na vikwazo, na zilikuwepo nyakati mlipokuwa katika hatari ya kuanguka na hata kunisaliti Mimi; lakini mlifahamu kuwa Nilikuwa katika harakati za kuwakomboa kila wakati? Kwamba kila wakati Nilikuwa napaza sauti Yangu kuwaita na kuwakomboa? Ni mara ngapi mmeanguka katika mitego ya Shetani? Ni mara ngapi mmejiingiza katika vishawishi vya wanadamu? Na tena, ni mara ngapi mmejikuta katika ugomvi usio na kikomo kati yenu kwa kukosa kuziachilia nafsi zenu? Ni mara ngapi miili yenu imekuwa katika nyumba Yangu ila roho zenu zikiwa kusikojulikana? Licha ya hayo, ni mara ngapi Nimewanyooshea mkono Wangu wa ukombozi; ni mara ngapi Nimewaonea huruma; ni mara ngapi Nimekosa uvumilivu wa kuziona hali zenu za kuhuzunisha za mateso? Ni mara ngapi … hamfahamu? Lakini leo kwa ulinzi Wangu, hatimaye mmezishinda shida zote na kuingia katika furaha pamoja Nami; hili ndilo dhihirisho la busara Yangu. Hata hivyo, likumbuke hili vyema! Ni nani kati yenu amewahi kuanguka na akaendelea kuwa thabiti? Ni nani kati yenu amewahi kuwa thabiti bila kuwa na nyakati za unyonge? Miongoni mwa wanadamu, ni nani amewahi kupokea baraka ambazo hazikutoka Kwangu? Ni nani kapitia misukosuko isiyotoka Kwangu? Inawezekana kuwa wale wote wanaonipenda hupokea baraka peke yake? Inawezekana kwamba misukosuko ilimpata Ayubu kwa kukosa kunipenda ila akanikana Mimi? Inawezekana kwamba Paulo aliweza kunihudumia kwa utiifu mbele Yangu kwa sababu aliweza kunipenda kwa dhati? Ijapokuwa mnaweza kushikilia ushuhuda Wangu, lakini je, kuna mtu kati yenu aliye na ushuhuda safi kama dhahabu ambayo haijatiwa najisi? Je, mwanadamu anaweza kuwa na uaminifu halisi? Ushuhuda wenu kuniletea furaha hakukinzani na “uaminfu” kwa sababu Sijawahi kumtarajia mtu yeyote kutoa zaidi. Kwa kufuata dhamira asilia ya mpango Wangu, nyinyi nyote mngekuwa “bidhaa duni—zisizokidhi kiwango.” Je, huu si ni mfano Niliowaambia “kuwaonea huruma”? Je, mnachoona si ni ukombozi Wangu?

Nyinyi nyote mnafaa kuvuta kumbukumbu zenu: Tangu mrejee katika nyumba Yangu, kuna yeyote kati yenu, bila kutafakari faida na hasara, amenifahamu sawa na Petro alivyonifahamu? Mmekariri Biblia kikamilifu, lakini je, mlijifunza chochote cha asili yake? Japo hivyo, bado mmeshikilia “mtaji” wenu, mkikataa kuziachilia nafsi zenu. Ninapotoa tamko, Nikiwazungumzia ana kwa ana, Ni nani kati yenu amewahi kuweka chini “nyaraka” zilizofunikwa kupokea maneno ya uzima ambayo Nimeyaweka wazi? Hamyajali maneno Yangu na wala hamyapendi. Badala yake, mnatumia maneno Yangu kama bombomu dhidi ya maadui wenu ili kudumisha nafasi zenu; hamjaribu hata kidogo kuyakubali maoni Yangu ili mnifahamu. Kila mmoja wenu anamwangazia sana mtu mwingine, nyinyi nyote ni “wasio bahili,” nyote “mnawajali wengine” katika kila hali; je, haya siyo mliyokuwa mnafanya jana? Na leo je? “Utiifu” wenu umepanda juu kwa alama kidogo, nyote mmekuwa wazoefu kiasi, mmekomaa kidogo na kwa sababu ya haya, “uoga” wenu Kwangu umeongezeka kwa njia fulani, na hamna hata mmoja “anayethubutu kutenda kwa wepesi.” Kwa nini mnaishi katika hali ya ubaridi wa kudumu? Ni kwa nini sifa nzuri hazipatikani kwenu? Enyi watu Wangu! Ya zamani yalipita kitambo; msiendelee kuyashikilia zaidi. Zamani mlishikilia msimamo wenu, leo mnapaswa kunipa utiifu wenu wa dhati, na zaidi mnafaa kuwa na ushuhuda mzuri Kwangu siku za usoni, na mtarithi baraka Zangu hapo baadaye. Hili ndilo mnapaswa kufahamu.
Japo Siko nanyi, Roho Wangu ataleta neema juu yenu. Kwa kutegemea hili, Natumaini mtaienzi baraka Yangu na mtaweza kujitambua. Msichukulie hili kuwa mtaji wenu; badala yake, mnatakiwa kujaza kinachokosekana ndani yenu kutoka katika maneno Yangu, na kutoka humu mpate vipengele vizuri mnavyovihitaji. Huu ndio ujumbe Ninaowaachia!
Februari 28, 1992
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa BwanaYesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungumwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni